0
Na Shomari Binda
        Musoma,

JUMLA ya Watoto 30 wanaoishi na Ulemavu Mkoani Mara wanatarajiwa kujiunga na Elimu ya Sekondari pamoja na mafunzo mbalimbali ya ufundi yakiwemo ya computer yanayowezeshwa na kituo cha kuhudumia watu wanaoishi na Ulemavu cha CBR-Mara kilicho chini ya Kanisa la Anglican Jimbo la Musoma.

Akinzungumza na Blog hii Ofisini kwake Mratibu wa CBR Dokta Hennry Yoggo alisema moja ya mipango ya kazi ya CBR kwa mwaka 2013 ni pamoja na kuwawezesha watoto wenye Ulemavu ambao wapo katika familia zisijojiweza kuhakikisha wanapata elimu ikiwemo ya ufundi ili kuja kujitegemea katika maisha ya baadae na kuepukana na utegemezi.

Alisema katika ofisi yake tayari wameshapokea maombi 30 ya watoto wenye ulemavu wakiwemo wa elimu ya sekondari pamoja na mafunzo mbalimbali ya ufundi ambao tayari wameshawafanyia utaratibu wa kuwalipia karo tayari kwa kujiunga na muhula wa masomo wa mwaka 2013.

Yoggo alisema Jamii inapaswa kuwajali watoto wanaoishi na Ulemavu katika kuwaandalia mazingira mazuri kikubwa ikiwa ni elimu ambayo itawawezesha kupata ujuzi ambao utawasaidia katika maisha na kuepukana na utegemezi kwa sababu tu wamezaliwa wakiwa na ulemavu.

" CBR-Mara katika kipindi cha mwaka 2013 tunazo program mbalimbali ikiwemo ya kuwasomesha watoto wanaoishi na ulemavu ikiwa na lengo la kuwatengenezea mazingira ya kielimu ambayo yatawasaidia kujishughulisha baada ya kuipata na kuepukana na masuala ya uegemezi na kujiona wa hali ya chini wakati wote.

"Watoto wanaoishi na ulemavu hawapaswi kutengwa kutokana na ulemavu walio nao bali ni wajibu wa jamii kushirikiana na kuona namna gani ambayo inapaswa kuchukuliwa ili kuwawezesha kupata elimu ambayo itakuwa msingi mkubwa katika maisha yao ya baadae,"alisema docta Yoggo.

Aidha Mratibu huyo wa CBR-Mara alidai licha ya kuwa na programu hiyo ya kusomesha watoto wanaoishi na ulemavu pia katika kipindi cha mwaka 2013 watakuwa na mpango wa kutoa elimu kwa Wanawake ya uzazi salama ili kujiepusha na ulemavu unaotokana na uzazi.

Alisema katika tafiti zilizofanywa imeonekana baadhi ya kina mama waamekuwa hawazingati mahudhulio ya kliniki hali inayosababisha kutokupata elimu juu ya uzazi salama na kupelekea kuleta matatizo katika kujifungua na kupelekea ulemavu wakati wa uzazi.

"Hii pia itakuwa ni program kubwa ya utoaji elimu kwa Wanawake juu ya uzazi salama na tumejipanua zaidi katika hili maana tutafika katika wilaya za Bunda,Butiama pamoja na musoma lakini kwa baadae tutafika katika maeneo yote ya mkoa wa Mara.

"Lakini elimu pia tutaitoa kwa wahudumu wa Afya pamoja na wakunga lengo likiwa kuhakikisha Mwanamke anapata elimu ya kutosha juu ya uzazi salama ili kuepukana na ulemavu ambao unaweza kutokea wakati wa kujifungua,"aliongeza.

Alidai baadhi ya Wanawake wamekuwa hawazingatii tiba za awali na mahudhurio ya kliniki wakati wa ujauzito na kupelekea kuzaliwa watoto wenye ulemavu.

Post a Comment