KAMANDA wa jeshi la polisi
mkoani Mara Ferdinand Mtui ametoa onyo kali kwa mtu yoyote
atakayesherehekea mwaka mpya kwa kuchoma moto ama kupiga mafataki usiku
wa leo ataishia mikononi mwa jeshi la polisi.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari ofisini kwake,Kamanda Mtui amesema jeshi la
polisi limejipanga vizuri kuhakikisha wale wote watakaoenda kinyume na
maelekezo wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Amesema
kuchoma moto barabarani ni kosa la jinai kama yalivyo makosa mengine na
kuwataka wananchi kuukaribisha mwaka mpya kwa amani na utulivu ili
kuepuka kuishia mikononi mwa polisi.
Kamanda
huyo wa jeshi la polisi mkoani Mara amesema askari wake wamejipanga
vizuri kukabiliana na mtu ama watu watakaotaka kuutumia mwanya wa
sherehe za mwaka mpya kufanya uhalifu na kuwataka wananchi kutoa
ushirikiano kwa jeshi hilo ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu.
Ameongeza
kuwa ili kuona namna walivyojipanga doria kali litaanza saa tisa mchana
katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mara na kudai yoyote aliyepanga
kutaka kufanya uhalifu aache maana ataishia mikononi mwa polisi.
Katika
hatua nyingine,kamanda Mtui amesema kuwa katika kuendelea na oparesheni
mbalimbali,jeshi hilo limefanikiwa kupataa bunduki aina ya SMG.NO.UC
5677-1998 ikiwa na magazine yenye risasi 12 iliyosalimishwa jirani na
kituo kidogo cha polisi Isenye Wilayani Serengeti.
Post a Comment
0 comments