ELIZABETH MWAKIJAMBILE AMBAYE PIA ALIINGIA TOP FIVE YA BSS 2013
NI POZI AMA TEGO
MOROMORO MAUNO!
ANAKWAMBIA HAPA KAZI TU.
WE MAINA
NI MWENDO WA KIUNO MAUNO WA MSHIRIKI WA BSS 2013 MAINA TADEI
Dj Mwarabu akiwa mtamboni
EMANUEL MSUYA AKITOA BURUDANI
HISIA PIA ZILITAFUTWA
TWENDE KAZI
MASHABIKI WA BURUDANI MJINI MUSOMA WAKIMYANYUA JUU KWA SHANGWE EMANUEL MSUYA MSHINDI WA BSS 2013
MSHINDI wa shindano la Bongo Star Search 2013 Emanuel Msuya
mwishoni mwa wiki amedhihilishia kwamba hakupendelewa kuibuka mshindi wa
shindano hilo baada ya kukonga nyoyo za mashabiki wa burudani mjini Musoma
katika show maalumu ya kuwashukuru mashabiki waliopigia kura iliyofanyika
kwenye ukumbi wa bwalo la polisi mjini hapa.
Katika show hiyo ambayo Msuya aliambatana na washindi
wengine walioiingia tano bora katika kinyang’anyiro hicho,aliwainua mashabiki
waliofika katika ukumbi huo mara baada ya kupanda jukwaani na kuanza kuimba
wimbo mapenzi wa bendi ya muziki wa dansi ya FM Academmy (Ngwasuma)uliowainua
mashabiki wote waliokuwepo ukumbini hapo.
Baada kumaliza kuimba wimbo huo Msuya hakuwarudisha vitini
mashabiki pale alipowaendezea shangwe na wimbo wake mpya wa leo ni leo ambao
ulionekana kupokewa vyema na mashabiki na kumfanya kila mmoja kutoondoka
jukwaani.
Wakizungumza na BLOG hii baadhi ya mashabiki wa burudani
walioshuhudia show hiyo ambayo ilionekana kama ya funga mwaka walimuelezea
mshindi huyo wa BSS kuwa ni moja ya vipaji ambavyo vilikuwa havionekani na sasa
vimeibuliwa.
Walisema Msuya anao uwezo mkubwa wa kulimiliki jukwaa na
kuimba na kusema asipoingiza mambo mengine ambayo yamekuwa yakiwapoteza
watangulizi wake katika shindano hilo atakuwa ni mmoj ya wasanii watakaofika
mbali kwa kufanya vizuri.
Kwa upande wake muandaaji wa burudani hiyo Mkurugenzi wa
Kayombe Entertainment&Promotion Dr Theophir Kayombo amewashukuru wakazi
wote wa Musoma na maeneo mengine ya nje ya Musoma kwa kumpa mapokezi makubwa
mshindi wa BSS 2013 pamoja na washiriki wengine walioingia tano bora alio ambatana
nao.
Amesema kwa kuwa ni msimamizi wa wasanii wengi wanaotoka
Mkoa wa Mara atahakikisha anamuongoza vyema Msuya ili aweze kufikia kiwango cha
juu zaidi na kudai ushauri zaidi wa kujenga kutoka kwa mtu yoyote unapokelewa ili
kumjenga msanii huyo.
Washiriki wengine walioambatana na Emanuel Msuya ni
Elizabeth Mwakijambile,Maina Tadei,pamoja na Amina Chibaba ambao wote waliimba
nyimbo zilizowapa ushindi katika kinyng’anyiro hicho sambasamba na wimbo wa
kila mmoja aliorekodi mara baada ya kumalizika kwa shindano hilo.
Post a Comment
0 comments