ASKOFU
Mkuu wa Kanisa la Romani Katoriki (RC) Dayosisi ya Mara Michael
Msonganzila ameiomba jamii kubadilika na kuachana na tabia mbaya ya
kuwahfanyia Ukatili Wanawake na Watoto kwa kuwa kitendo cha ukatili
licha ya kuwa kinamfanya muhanga kupata madhara na hata kifo lakini pia
kina mdhalilisha.
Akizungumza
na Wananchi wa Vijiji vya Borega na Nyiboko Kata ya Kisika Wilayani
Serengeti katika maazimisho ya siku 16 za kupinga Ukatili,Askofu
Msonganzila alisema kuendelea kufanyika kwa vitendo vya Ukatili kwa
Wanawake na Watoto kunapelekea kuendelea kuwa na familia masikini
kutokana na kushindwa kufanya shughuli za kiuchumi zikiwemo za kilimo.
Alisema
vitendo vya Ukatili vimekuwa vikiendelea kila kukicha katika familia
nyingi
na kudai ili kukomesha vitendo hivyo hakuna budi kuwa na nguvu ya
pamoja baina ya Serikali, Taasisi za kidini na Mashirika yasiyo ya
Kiserikali ili kuweza kukomesha hali hiyo ya vitendo vya Ukatili.
Askofu
Msonganzila alisema katika jamii viko vitendo mbalimbali vya Ukatili
vikiwemo vya kimwili,kisaikolojia na kijamii ambavyo vinafanywa na
kufanya jamii kuwa dhoofu kwa mambo mengi na kukosa haki nyingi za
msingi ambazo muhanga anastahili kuzipata.
Alisema
kung'ang'ania mila potofu ya ukeketaji kunaendelea kuwafanya Wasichana
kulazamishwa kukeketwa na kuwaacha na maumivu makali na hata kupelekea
vifo kitu ambacho bila elimu ya kutosha kuendelea kutolewa mabadiliko ya
kweli ya kukomesha vitendo vya ukatili haita fanikiwa.
Msonganzila alidai ili kuweka nguvu ya pamoja katika
kutokomeza vitendo vya Ukatili kwenye jamii,Kanisa Katorika Jimbo la
Musoma litaendeleza jitihada za kutoa elimu juu ya athari za Ukatili kwa
kutumia Idara yake ya Haki na Amani pamoja na Idara ya Mipango na
Maendeleo kwa kufungua matawi kila Parokia ili kutoa elimu kwa jamii.
kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Musoma Angelina Mabula alilishukuru
Kanisa Romani Katoriki pamoja na Taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali
kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha elimu
madhubuti inatolewa ili
kuhakikisha vitendo vya ukatili vinaondoka kwenye jamii.
Alisema
ni vyema kuyatumia maazimisho ya siku 16 za kupinga Ukatili wa kijinsia
kwa kufanya tathimini ya kweli ili kuondoa na kukomesha vitendo vya
Ukatili vikiwemo kupiga Wanawake,Kukeketa Wasichana,kuoza
wasichanawadogo,kutoa watoto wa kike shuleni na kuwaoza pamoja na
kutelekeza watoto.
Post a Comment
0 comments