CHAMA CHA MPIRA WA
MIGUU MKOA WA MARA – FAM
Affiliated to TFF
YAH: MAAMUZI YA TFF,
KAMPENI ZA WAGOMBEA NA UCHAGUZI.
Leo tarehe 14/6/2016, Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM) kwa mujibu
wa Katiba ya FAM, Kanuni za uchaguzi TFF na baada ya kupokea maamuzi ya malalamiko toka TFF, katika barua ya
tarehe 13/6/2016 yenye kumbukumbu namba TFF/ADM/LM.39/2016 inapenda kuwatangazia wanachama wa FAM, wadau wa michezo na umma kwa
ujumla kupitia magazeti, radio, TV na mbao za matangazo kuwa wagombea wafuatao
wamekidhi vigezo kwa mujibu wa katiba ya
FAM na Kanuni za uchaguzi za TFF na wanapewa nafasi ya kugombea nafasi kama
walivyoomba; wagombea hao ni;
- MICHAEL Richard Wambura Nafasi ya mwenyekiti.
- MAGATI Zamberi Francis Nafasi ya makamu mwenyekiti.
- SAMWELI Silas Nafasi ya katibu.
- REVOCATUS Mashauri Kuboja Nafasi ya Katibu.
- BENARD S. Sakira Nafasi ya katibu.
- EJAGA Mahamba Nafasi ya mweka hazina.
- MOSES Timoth Kimwaga Nafasi ya mweka hazina
- MUGISHA M. Galibona Nafasi ya mjumbe mkutano mkuu.
- MUGETA Mtete Nafasi ya mjumbe mkutano mkuu
- YAMO Odemba Kagose Nafasi ya mjumbe mkutano mkuu
- ELIUD William Bwire Nafasi ya mwakilishi wa vilabu.
- KILIGINI Mabalaja Bandoma Nafasi ya mwakilishi wa vilabu.
- GORDON P.M. Mumbara. Nafasi ya mwakilishi wa vilabu.
Wagombea tajwa hapo juu wanaruhusiwa kuanza kampeni kama inavyoonyesha
katika ratiba iliyotolewa tarehe 11/4/2016, na kwamba uchaguzi ni tarehe
18/6/2016.
Pia TFF imemwengua mgombea ndugu
Sospiter Masambu Aliyekuwa anagombea nafasi ya ujumbe wa mkutano mkuu TFF kwa
kosa la kukiuka katiba ya FAM ibara ya 7 Kifungu cha 2(d).
Nawatakieni wagombea wote kampeni njema zenye kufuata
maadili kwa mujibu wa sheria za Tanzania.
“MICHEZO NI FURAHA, AFYA NA AJIRA”
WAKILI OSTACK
MLIGO
MWENYEKITI KAMATI YA UCHAGUZI FAM
Post a Comment
0 comments