Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini Tanzania (UTPC), Deogratius Nsokolo, akifungua Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (Union of Tanzania Press Club- UTPC) unaofanyika La Kairo Hotel Jijini Mwanza kwa siku mbili kuanzia leo Oktoba 06,2016 na Oktoba 07,2016.
Mkutano huo wenye kauli mbiu ya "Viongozi Mustakabali wa Press Clubs Upo Mikononi Mwenu"unajadili masuala mbalimbali ikiwemo Mpango Mkakati wa UTPC kwa mwaka 2016/20 uliofadhiliwa na Shirika la "The Swedish International Development Cooperation Agency (SIDA)"
Wajumbe mbalimbali wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC
*****************************************
Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kuusoma na kuuelewa vyema mswada sheria ya huduma ya vyombo
vya habari 2016, uliowasilishwa na Serikali bungeni mjini Dodoma, kwa ajili ya kutoa maoni yao juu ya mswada huo.
Rai hiyo imetolewa na Rais wa Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC Deo Nsokolo,
wenye Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Muungano huo, unaofanyika kwa siku mbili Jijini Mwanza kuanzia leo.
Nsokolo amesema tayari kamati ya bunge
imekwisha kabidhiwa mswada huo kwa ajili ya kukusanya maon hivyo ni
vyema waandishi wa habari ambao wanaguswa moja kwa moja
na mswada huo, wakausoma kiundani na kisha kutoa maoni yao kabla ya kuwasilishwa bungeni ili kuidhinishwa.
Akiwasilisha mswada huo katika bunge lililopita, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, alisema ikiwa mswada huo utapitishwa na bunge kuwa sheria,
utasaidia kuleta mageuzi makubwa ya kitaaluma kwa wanahabari pamoja na huduma za vyombo vya habari nchini.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
SHUKRANI KWA GEORGE BINAGI WA BINAGI GROUP NA KADAMA MALUNDE WA MALUNDE 1 BLOG KWA PICHA NA TAARIFA KUTOKA KWENYE MKUTANO

Post a Comment
0 comments