 |
MKUU wa
wilaya ya Bunda, Lyidia Bupilipili, amezindua uandikishaji wa bima ya afya kwa
watoto walio chini ya miaka 18 huku akitoa wito kwawazazi na walezi
kuhakikisha wanatimiza wajbu wao kwa kuhakikisha kila anayelengwa anakatiwa ili
aweze kupata huduma ya afya kwa uhakika.
Akizungumza
kwenye uzinduzi huo uliofanyika kwenye kituo cha afya Bunda na kuhudhuliwa na
wazazi,walezi na viongozi mbalimbali wakiwemo madiwani, alisema upo umuhimu
mkubwa wa kuhakikisha kila mtoto anapata bima hiyo.
Amesema
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umekuwa na malengo mazuri ya kuhakikisha
inafikisha huduma bora za kiafya kwa wananchi kwa michango nafuu na huduma hii
inayowalenga watoto ni wajibu wa kila mzazi na mlezi kuipa umuhimu wa pekee.
|
Bupilipili
amesema kiasi cha shilingi 50400 kinacholipwa kwa mwaka mmoja kwaajili ya
kupata kadi ya mtoto aliye na umri chini ya miaka 18 itamsaidia kupata huduma
hata pale mzazi anapokuwa hana pesa na kujiepusha na changamoto mbalimbali.
Amesema
ugonjwa hauna taarifa na watoto wamekuwa wakiugua hivyo pale mzazi anapokuwa
hana fedha kwa wakati anajikuta anaangaika kuomba fedha za kumtibia lakini
anapokuwa na kadi ya bima anapata huduma mahali popote.
 |
“ Wazazi na
walezi tutimize wajibu wetu kwa kuhakikisha tunawakatia watoto wetu kadi za
abima ya afya ili wawe na uhakika wa matibabu kwa wakati wowote na sio kusubili
mtoto ameugua tunaanza kuomba fedha za matibabu kila mahala.
“
Niwashukuru pia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kwa kuleta utaratibu huu kwa
watoto wetu na kwa gharama nafuu kwa mwaka lakini ni vyema mkayaangalia na
makundi mengine kwenye jamii”,amesema Bupilipili.
|
 |
Meneja wa
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoa wa Mara,Dk. Daud Zakaria Bunyinyiga, amesema
uongozi wa wilaya ya Bunda umelipokea zoezi la uhamasishaji wa usaji wa watoto
walio na umri chini ya miaka 18 kujiunga na bima ya afya na zoezi hilo limeanza
vizuri.
Amesema
mtoto anapokatiwa bima ya afya kwa gharama ya shilingi 50400 kwa mwaka anapata
huduma kwenye hospitali,vituo vya afya na zahanati zaidi ya 700 nchini hivyo wazazi
na walezi wapokee huduma hiyo kwa kuwa ina umuhimu mkubwa. |
 |
Mzazi akiweka fomu baada ya kuandikishwa |
Burudani pia ilihusika kwenye uzinduzi
Wanafunzi wakifatilia uzinduzi
Meneja wa NHIF mkoa wa Mara,Dr.Daud Zakaria Bunyinyiga, akizungumza kwenye uzinduzi huo
Mzazi akiandikishwa

S
Mkuu wa wilaya ya Bunda,Lyidia Bupilipili akizungumza kwenye uzinduzi huo
Sister wa kituo cha yatima cha Mtakatifu Fransisko kilichopo Bunda akiwa na mmoja wa watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho waliokatiwa kadi na mkuu wa wilaya
Sister Anta Heshaj, akishukuru baada ya watoto wanaolelewa kwenye kituo cha Mtakatifu Fransisko kupewa kadi za afya na mkuu wa wilaya ya Bunda
Post a Comment
0 comments