0


JESHI la polisi mkoani Mara limesema limejipanga kuhakikisha ulinzi wa kutosha dhidi ya uhalifu na wahalifu unaimalishwa ili kuwafanya Wananchi washerekee kwa amani sikukuu ya krismass na mwaka mpya.

Akizungumza na BLOG HII ofisini kwake,kamanda wa polisi mkoani Mara Ferdinand Mtui amesema kikosi kazi kutoka ndani ya jeshi la polisi kimeundwa na kukabidhiwa majukumu kuhakikisha hali ya amani inakuwepo katika kipindi hicho.
 
Amesema mtu yoyote ambaye atakuwa na lengo la kutumia mwanya wa sikukuu kkufanya uhalifu maishio yake yatakuwa mikononi mwa polisi.
 

Post a Comment