0


Kundi la Muziki wa Taarabu la TOT Plus usiku wa leo litatoa burudani kwa wakazi wa Mji wa Musoma na vitongoji vyake katika ukumbi wa bwalo la Magereza ikiwa ni sambamba na uzinduzi wa album mbili mpya  kwa pamoja na nyimbo za zamani.

Akizungumza na blogu hii mara baada ya kuwasili mjini hapa baada ya kufanya show ya nguvu mjini Bukoba,mratibu wa ziara ya kundi hilo katika mikoa ya kanda ya ziwa,Gasper Tumaini amesema kazi itakayofanyika leo ni kuhakikisha wanatoa burudani ya haja kwa wakazi wa Musoma na vitongoji vyake ama ilivyo ada ya kundi hilo.

Amesema kundi la TOT Plus linafahamika katika suala zima la burudani na kuahidi kuhakikisha watoa burudani ambayo haijawahi kupatikana katika siku za hivi karibuni kwa wakazi wa Mkoa wa Mara hususani katika mji Musoma.

Gasper amesema album ya kwanza itakayozinduliwa leo inakwenda kwa jina la Mjini Chuo Kikuu ikiwa na jumla ya nyimbo 6 ikiwemo nyimbo iliyobeba album hiyo inayokwenda kwa jina  hilo la mjini chuo kikuu

Amesema album ya pili itakayozinduliwa hii leo inakwenda kwa jina la Full Stop ambayo pia ina nyimbo sita ikiwemo nyimbo iliyobeba album hiyo ya full stop pamoja na nyimbo nyingine kama vile rudi mpenzi pamoja na utakoma kulinga.

Amedai licha ya nyimbo hizo pia wapenzi wa burudani wa muziki wa taarabu wa kundi hilo la TOT Plus watapata nafasi ya kusikiliza nyimbo ambazo zinapatikana katika album yao iliyotangulia inayokwenda kwa jina la TOP IN TOWN.

Gasper ameongeza kuwa show ya leo itakuwa ya kipekee kwa wakazi wa Mji wa Musoma kwani wameongozana na kikundi cha vijana wa show ambao watanogesha jukwaa la TOT katika ukumbi wa bwalo la Magereza kwa kufanya show ya nguvu.

Amekitaja kiingilio ambacho kitawafanya wapenzi wa muziki wa taarabu kushuhudia burudani ya kundi hilo kitakuwa ni shilingi ni shilingi elfu saba (7000).

Post a Comment