Na Shomari Binda
Musoma,
Musoma,
WATU waNNE wamefariki dunia katika matukio matatu tofauti yakiwemo ya kuawa,kujinyonga na kuchomwa kisu mkoani Mara.
Katika tukio
la kwanza lilotokea juzi watu wenye hasira katika kijiji cha Nyabirekera
wilayani Serengeti,wamemuuwa mkazi mmoja wa kijiji hicho kwa kumpiga mawe kisha
kuuchoma moto mwili wake baada ya kumtuhumu kujihusha kwa imani za kishirikina.
Kamanda wa
polisi mkoani Mara,kamishina Msaidizi Mwandamizi Absalom Mwakyoma,alimtaja
marehemu kuwa ni Nyabuke Maheri,ambaye anakisiwa kuwa na umri wa miaka 68.
Hata hivyo
kamanda Mwakyoma,alisema ingawa bado chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa lakini
ametoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi badala
yake wanapowakamata wahalifu kwa makosa yoyote wawafikishe katika vyombo dola
ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Mjini Musoma Mwanamke mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja mkazi wa
Buhare Mgaranjabo, Manispaa ya Musoma alikutwa amekufa
kwa kunyongwa na kanga shingoni na mwili wake kutupwa kichakani na
watu wasiojulikana huku chupi yake ikiwa imechanwa.

Taarifa ilisema kando ya mwili wa marehemu ilikutwa chupi, skin
tight vimechanwa, dumu la kuchotea maji likiwa mita 20 tokea mwili
ulipokuwa.
Ilidaiwa nywele za marehemu zilikutwa zikiwa zimefungwa kwenye
kijiti kichakani hapo na kanga ikiwa shingoni huku ulimi wake ukiwa
nje na kinyesi pembeni.
Kutoka wilayani Tarime,kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa Tarime na Rorya Justus Kamugisha,alisema mtu mmoja Genkuri Chacha(34) aliuawa baada ya kuchomwa kisu na mdogo wake Nyengwe Chacha(25).

Alisema chanzo
cha tukio hilo ambalo limetokea katika kitongoji cha Kwigongo kijiji cha Itiryo
februari tatu mwaka huu lilisababishwa na kugombea ardhi ndipo mgodo wa
marehemu alimchoma kisu kaka ake katika mkono wa kulia na kufa hapo hapo.
Hata hivyo
kamanda Kamugisha alisema kuwa baada ya tukio hilo mtuhumiwa huyo alikimbia
hadi alipkutwa jana feb nne akiwa amekufa kwa kujinyonga katika shamba
walilokuwa wakigombania.
Post a Comment
0 comments