0

KAMANDA MWAKYOMA

MKUU WA MKOA WA MARA JOHN TUPPA



Na Shomari Binda
         Musoma,    


SERIKALI mkoani Mara ilisema kamwe haitawavumilia wanasiasa ambao wamekuwa wakitumia majukwaa  ya kisiasa kuchochea chuki,vurugu huku wakihamasisha wananchi kuvunja sheria za nchi.


Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Mara Bw John Tupa,wakati wa kukabidhi piki piki 12 ambazo zimetolewa na Serikali kwaajili ya kusadia uhimalishaji wa ulinzi katika mradi wa ukaguzi wa tarafa ambazo zimetolewa kwa wilaya za mkoa wa Mara.

Alisema wanasiasa kwa sasa badala ya kuhubili amani na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo kwa Wananchi ili kujikomboa kiuchumi wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa lugha zisizo za kiungwana na kupelekea kuzuka kwa vurugu katika jamii.


Kwa sababu hiyo aliwataka viongozi hao wa vyama vya siasa kutumia nafasi zao katika kuhamasisha shughuli za Maendeleo kwa Wananchi.

Tuppa pia aliwaomba viongozi wa madhebu ya dini kutumia nafasi  zao kuhubiri upendo na amani miongoni mwa jamii na luachana na vitendo vya uhalifu ili kuweza kuishi kwa amani pamoja na kuheshimu sheria za nchi. 


Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa wa Mara ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa huo alisema Mkoa wake hautawavumilia askari polisi wanatumia vyombo vya usafiri vya jeshi hilo kwaajili kukusanyia rushwa na kufanya biashara haramu zikiwemo za uvushaji wa dawa za kulevya.

"Pikipiki hizi zimetolewa kwa kazi iliyokusudiwa ya kukusanya taarifa katika tarafa hivyo naomba zitumiwe kwa kazi iliyokusudiwa na si vinginenyo.

"Iwapo Serikali itapata taarifa kuwa pikipiki hizi zinatumiwa kwa kusaidia vitendo vya uhalifu na kwenda kupaki kwenye vilabu vya pombe na kufanya ulevi itafadhaika sana lakini askari atakayefanya hivyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake,"alisema Tuppa.


Kuhusu wananchi,mkuu huyo wa mkoa wa Mara,alisema hata jeshi hilo likapewa kila kitendea kazi lakini ni wajibu wanajamii kushirikia katika kupambambana na vitendo vya uhalifu yakiwemo mauaji ya kikatili ambayo yamekuwa yakitokea katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mara.


Naye kamanda wa polisi mkoa wa Mara kamishina msaidizi mwandamizi Absalom Mwakyoma,alisema piki piki hizo ni sehemu piki piki 164 za ukaguzi wa tarafa kwa kuzuia uhalifu mradi ambao uliziinduliwa na mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema lengo likiwa ni kupambana na wahalifu na uhalifu nchini.

Post a Comment