0
MWENYEKITI WA CCM MKOA WA MARA CHRISTOPHER SANYA KUSHOTO AKIJULIA HALI ZA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA DDH MJINI BUNDA


Na Shomari Binda
          Musoma

Chama cha Mapinduzi Mkoani Mara (CCM) kimesema kitayafanyia kazi maazimio ya Mkutano Mkuu wa nane wa Chama hicho uliofanyika Mkoani Dodoma kwa kufatilia utekelezaji wa ilani ya CCM ikiwa ni kufatilia sekta ya Elimu,Afya,Maji pamoja na huduma nyingine ambazo jamii inastahili kuzipata kama ilani inavyoeleza.

Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Christopher Sanya alipokuwa akizungumza na BLOG hii kuhusiana na miaka 36 ya CCM na namna ambavyo Chama hicho kimejipanga katika kuhakikisha yale yote yaliyoelezwa katika ilani yanatekelezwa katika kila idara na kuondoa vikwazo ambavyo vinawapata Wananchi pale wanapofatilia huduma.

Alisema maazimio ya Mkutano wa nane ni kuhakikisha kila Kila kiongozi wa Chama katika nafasi yake anasimamia ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kufatilia utekelezaji wake na kuacha kukaa kimya pale wanapoona watendaji wanashindwa kuitekeleza na kupelekea kuwapa mwanya baadhi ya watu kusema hakuna kitu kinachofanyika.

Alisema kwa upande wa Mkoa wa Mara tayari wameshaanza kukutana na viongozi wa idara mbalimbali chini ya Mkuu wa Mkoa kuona na namna utekelezaji wa ilani unavyo tekelezwa kuanzia Elimu,Afya,Maji pamoja na sekta nyingine.

"Ifahamike Chama cha Mapinduzi (CCM) ndio Chama Tawala ambacho kinasimamia utekelezaji wa yale yaliyoandikwa katika ilani kutokana na maelekezo ya Mkutano Mkuu uliofanyika Mkoani Dodoma lazima tuyafuate kwa kufatilia kwa karibu jinsi ilani inavyotekelezwa katika kila idara.

"Kuna malalamiko yanatolewa katika idara ya afya kwamba wazee pamoja na watoto walio na umri chini ya miaka 5 hawatibiwi bure kama ambavyo ilani inavyoeleza tutakutana na Mkuu wa Mkoa kulingalia sula hili kwa namna ya pekee ili kama suala hilo lipo kuona namna ambayo itawekwa vizuri kuona wazee pamoja na watoto walio na umri chini ya miaka 5 wanapata huduma bure.,alisema Sanya.

Alisema si vyema kuona wazee wakinyanyasika kupata huduma za afya zinazostahili wanapokwenda katika hospitali na vituo vya afya kwa kuwa katika ilani imeeleza wazee wote watapata huduma za afya bure bila kutoa gharama yoyote hivyo lazima suala hilo lisimamiwe na kuondoa kikwazo cha wazee kutokupata huduma.

Alidai ili kufatilia utekelezaji huo kwa karibu watakuwawakikutana kila baada ya miezi mitatu kuona namna ilani ilivyotekelezwa kwa kipindi hicho na pale kwenye mapungufu ya utekelezaji kuona namna ambavyo itaboleshwa na kuleta tija katika utekezlezaji.

Akizungumzia hali ya kisiasa Mkoani Mara,Mwenyekiti huyo wa Chama cha Mapinduzi Mkoani hapa alisema mara baada ya Uchaguzi ndani ya Chama hicho kazi iliyopo sasa ni uhimalishaji wa Chama kwa kufanya mikutano ya hadhara na ile ya ndani ili kukijenga zaidi kabla ya kuingia katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka 2014 na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Alisema licha ya kuwepo na ushindani wa vyama vya kisiasa wamejipanga kukabiliana na hali hiyo  kwa kuendelea kukiimalisha Chama na kuweka utaratibu mzuri wa kufanya mikutano na kila kiongozi kuitumia nafasi yake kutekeleza majukumu huku akikisitiza kufanya ufatiliaji wa ilani na kuona utekelezaji wake kwa kuwa ndio siraha katika chaguzi zinazokuja mbele.

Post a Comment