ASKARI WA USALAMA BARABARANI WAKITOA MSAADA
Ajali mbaya imetokea asubuhi ya leo majira ya saa 2 kwenye
barabara ya majita karibu na makazi ya mkuu wa mkoa wa Mara baada ya gari aina
ya VX land cruser namba T 901 AHH kuigonga pikipiki iliyokuwa ikitoka maeneo ya
mjini musoma kuelekea kamnyonge.
Kamera yetu imemshuhudia majeruhi wa ajali aliyedaiwa kuwa
ni abiria akiwa anavuja damu nyingi kichwani huku akipumua kwa shida na muda
mchache askari wa kikosi cha usalama barabarani walifika eneo la tukio na
kumchukua kwa ajili ya kumuwahisha hospitali.
Mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo kabla ya camera ya bloog
hii kufika eneo la tukio muda mchache wamesema dereva wa pikipiki ambaye
alidaiwa kupakia abilia alitaka kulipita gari hilo na kuingia eneo la gari hali
iliyopelekea kutokea kwa ajali hiyo.
Mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo dereva wa pikipiki Wambura
Matiku aliyekuwa nyuma ya pikipiki iliyopata ajali aliiambia blog hii dereva wa
pikipiki mara baada ya kulipita gari
hilo aliwahi kuingia upande wa gari na kutokea kwa ajali hiyo.
Hata hivyo jeshi la polisi mara baada ya kumuwahisha
majeruhi huyo hospitalini walirejea eneo la tukio na kupima ili kubaini chanjo
cha ajali hiyo huku Kamanda wa polisi Mkoa wa Mara Ferdinand Mtui akiahidi
kuhitolea taarifa mara baada ya kubaini chanzo cha ajali hiyo
Post a Comment
4 comments
Please sio ubinadam kuweka Picha Kama hizo kwenye vyombo vya habari, tunawezasoma habari yako bila Picha za huzuni Kama hizo, mpe stara huyo mtu alielala hapo chini, jaribu kuuthamini mwili wake. Na fikiria ingekuwa ni maiti yako ungependa ianikwe hadharani kiasi hicho?? Tujifunze kutoa habari bila kutumia miundombinu ya kupata wasomaji iliyopitwa na Wakati.
Ushauri wangu, ondoa hizo picha. Mpe heshima Marehemu na ndugu na jamaa zake.
Waendesha piki piki wafute sheria za barabarani hii itachangia kupunguza ajali