0


MIRADI mbalimbali inayoendelea kutekelezwa mkoani Mara imeelezwa kuwa chini ya ilani ya chama cha mapinduzi (CCM)ikiwa inaoongozwa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Jakaya Kikwete ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho ya mwaka 2010.

Kinana aliyasema hayo baada ya kusikia baadhi ya viongozi wa vyama vua Siasa Wilaya ya Musoma wakidai yale yote yanayofanyika katika Wilaya hiyo ikiwemo miradi ya maji,barabara na shule ni kazi inayofanywa na vyama vya upinzani.

Katika mkutano wa hadhara wa kuhitimisha ziara ya siku sita mkoani Mara katika viwanja vya shule ya msingi Mukendo,alisema yale yanasemwa kwenye majukwaa na vyama vya upinzani ni uongo wa mchana kwa kuwa shughuli zote zinazofanyika ni utekelezaji wa Ilani na fedha zinatolewa na Serikali inayoongozwa na CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete.

Alisema mradi mpya wa maji Musoma utakao ghalimu kiasi cha zaidi ya bilioni 40 ulibuniwa na serikali ya awamu ya nne kabla ya kuingia madarakani mwaka 2004 na kwamba baada ya kuingia madarakani Rais wa awamu hiyo mhe. Jakaya Kikwete alifanikiwa kuanzisha mradi huo katika miji 14 nchini ikiwemo manispaa ya Musoma mnanamo mwaka 2005.

 ‘’Mradi huu wa maji mnao uona pale Bukanga ni mradi wa serikali upo kwenye ilani ya CCM hivyo maneno mengine mnayo ambiwa yafatilieni na msiwe wepesi wa kuwasikiliza watu wanaowadanganya’’alisema Kinana.

Aliongeza kuwa mradi huo umegharimu jumla ya shilingi bilioni 48 na kwamba utatoa huduma ya maji kwa asilimia 95 ya wakazi wa Musoma huku jumla ya kilomita 140 za mabomba ya maji yanatarajiwa kusambazwa ili Wananchi wapate maji kwa uhakika.

Hata hivyo alibainisha kuwa baadhi ya miundombinu inayoendelea kutekelezwa mikoa mbalimbali ikiwemo Arusha,Dodoma,Mtwara,Mbeya na Mara inatengenezwa kwa kiwango cha lami alisema ni ilani ya  Serikali iliyoadhimia kujenga miundombinu hiyo katika miji 18 nchini.

‘’Kwa hiyo wewe unalipia laki mbili hadi tatu kuunganishiwa umeme kwa watu wa mjini huku watu wa vijijini wanalipia  Tshs.36000 tu kupelekewa umeme kwa sababu watu wa kijijini uwezo hao wa kulipa umeme ni mdogo ,kuna zaidi ya vijiji 5000 nchini vinagawiwa umeme’’aliongeza.

Alitaja mradi utakaogharimu fedha nyingi kuwa wa Afya kufuatia muendelezo wa hospitali ya rufaa ya Kwanga mjini hapa iliyoanzwa kujengwa mwaka 1975 kipindi cha uongozi wa Baba wa Taifa mwl. Nyerere kwa nguvu za wananchi ambapo ulisimama baada ya vita vya Uganda kutokea  na

Alisema mradi huo unatarajia kuanza wiki ijayo na utajengwa kwa shilingi bilioni 14 namilioni 400 kufuatia maombi yake ya kuongezewa bilioni10 kutoka serikalini ilikufanikisha mradi huo.

Katika ziara hiyo pia aliongozana na katibu muenezi wa CCM mhe. Nape Nauye pamoja naye katibu mkuu wa UWT.mhe.Anna Makilagi na baadhi ya viongozi wengine wa chama hicho.

Post a Comment