MBUNGE wa jimbo la Musoma mjini Vicent Nyerere amesema kuwa
idara nyeti za serikali mkoani Mara ndizo zinazoongoza kwa kudaiwa deni kubwa
la maji ikiwemo ikulu ndogo.
Mbunge huyo aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akiwahutubia
maelfu ya wananchi wa mji wa Musoama na vitongoji vyake katika mkutano wake wa
hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule sekondari Mara.
Nyerere alisema kuwa ofisi ya mkuu wa mkoa yaani nyumbani
kwa mkuu wa mkoa inadaiwa shilingi 10,592,668.70, Magereza mkoa wanadaiwa shilingi 1,275,585.97,mganga
mkuu wa mkoa anadaiwa shilingi 35,352,117,50,wakala wa barabara mkoa wanadaiwa
shilingi 920,373,00.
Alizitaja idara nyingine zinazodaiwa deni hilo kubwa kuwa ni
pamoja na JWTZ Makoko wanaodaiwa shilingi 1,180,466.00,shirika la umeme Tanesco
wanadaiwa shilingi 2,193,027,55 ,ofisi
ya kamanda wa polisi Mara wakidaiwa shilingi 91.361,438.00
Alisema kuwa kama pesa hizo zingekuwa zimelipwa kwa mamlaka
ya maji Musoma ,Muwasa ingeweza kujiendesha
ambapo alisema anashangazwa na wasimamizi wa idara hizo kwa kulipa
madeni hayo wakati serikali ikituma pesa nyingi.
‘’Nataka niwaambie nakwenda bungeni nitapeleka hoja binafsi
ya kutaka kufahamu ni kwa nini idara hizo hazilipi bili ya maji kwa Muwasa
maana hii ni kuzidi kudhoofisha idara hiyo’’alisema mbunge huyo.
Alisema kuwa kama pesa hizo zingekuwa zimelipwa kwa Mamlaka
ya Maji Musoma (Muwasa) ingeweza kujiendesha
ambapo alishangazwa na wasimamizi
wa idara hizo kwa kutolipa madeni hayo wakati Serikali ikituma pesa nyingi.
Kwa upande wake meya wa manispaa ya Musoma Alex Kisurura
alisema kuwa wananchi wa Musoma wanachohitaji ni maendeleo na wala si porojo za
akina Nape na Kinana hivyo wananchi watafakali wenyewe na kuona mahali ukweli
ulipo.
Meya huyo aliwaambia
wananchi hao kuwa Chama hicho kitaendelea kuwatumikia Wananchi kwa maana
walikiamini na wakakichagua hivyo hakitawaangusha bali waendelee kukiamini.
‘’Nawaambieni leo nimesaini mikataba mitatu ofisini kwangu
ya matengenezo ya barabara katika maeneo mbalimbali ya
Nyakato,Kwangwa,Nyamatare na hivyo wananchi msihofu achaneni na uongo wa Nape
CCM sasa haina sera kila kukicha ni kuisema chadema tu hawazungumzi namana ya
kukinusuru chama chao’’alisema Kisurura.
Post a Comment
0 comments