0
 MWILI wa aliyekuwa askari wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Mara na mdogo wa Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini na Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo,marehemu Dinna Faru Muhongo,atazikwa kesho kwenye makaburi ya Menonite mjini Musoma baada ya leo kutolewa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti na kupelekwa nyumbani kwao mtaa wa kawawa
 Katika ratiba iliyotolewa na msemaji wa familia,Dk.Musuto Chirangi,saa 3 asubuhi mwili wa marehemu utatolewa nyumbani kuelekea kwenye viwanja vya kikosi cha kutuliza ghasia FFU maeneo ya Kamnyonge kwaajili ya kutolewa heshima za kijeshi kisha kupelekwa kwenye Kanisa la Menonite Jimbo la Mara kwaajili ya ibada kisha kupelekwa makaburini kwaajili mazishi.
 Hapa mwili ukitolewa chumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya mkoa wa Mara na jeshi la polisi kwaajili ya kupelekwa nyumbani
 Mwili ukitolewa kwenye gari kuingizwa ndani

 Mwili ukipelekwa ndani
 Askari wa usalama barabarani akielekeza njia

 Mwili ukiingizwa ndani
 Mwili ukiwa umefikishwa ndani
 Maafisa wa polisi wakishauliana jambo baada ya kufikisha mwili nyumbani
 Mchungaji akitoa neno kwenye ibada ya jioni
 Waombolezaji wakiwa msibani


 Dk.Musuto Chirangi akiandaa ratiba ya mazishi
Post a Comment