0

WAZIRI wa Nishati na Madini na Mbunge wa Jimbo la Musoma mjini,Profesa Sospeter Muhongo,amewashukuru wananchi wa Musoma mjini,jeshi la polisi na watanzania kwa ujumla kwa kumpa ushirikiano kwenye msiba wa mdogo wake koplo Dinna Faru Muhongo,ambaye amezikwa leo kwenye makaburi ya Menonite mara baada ya kuagwa kutolewa heshima za kijeshi na ibada iliyofanika kwenye Kanisa la Menonite Jimbo la Musoma.

Muhongo amesema yeye hakuwepo wakati msiba ulipotokea lakini wananchi wa Musoma na jeshi la polisi wamefanya kazi kubwa na alipofika alikuta mambo yote yakiwa yamekamilika na hiyo imeonyesha namna kulivyo na ushirikiano na upendo.

Waziri Muhongo amesema ni vyema ushirikiano huo ukaendelezwa na jamiii ni kushirikiana kwenye matatizo na shughuli nyingine za kijamii na kuw wamoja ndio kunaweza kufanisha mambo.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Mara,Jafari Muhamed,amesema amempoteza mpiganaji na kudai hiyo ni kazi ya Mungu na kushukuru ushirikiano ambao wananchi wameutoa na kufanikisha kumpumzisha mpiganaji huyo kwenye nyumba yake ya milele.
 Mwili ukitolewa nyumbani




 Mwili ukielekea kikosi cha kutuliza ghasia FFU kwaajili ya kutolewa heshima za mwisho

 Maeneo ya FFU
 Mwili ukiingia viwanja vya FFU
 Familia ikiingia
 Maandalizi ya kuanza kutolewa heshima za kijeshi


 Waziri Muhongo akiwa anatafakari jambo
 Askari wa kikosi cha usalama barabarani wakiwa eneo la viwanja vya FFU
 Kamanda wa polisi mkoa wa Mara akitoa shukrani kwa wananchi waliotoa ushirikiano
 Msemaji wa familia Dk.Musuto Chirangi akitoa shukrani
 Askari wakitoa heshima za mwisho


 Waziri Muhongo akitoa heshima
 Uchungu wa Kufiwa

 Mkuu wa mkoa wa Mara Dk.Charles Mlingwa pia alitoa neno
 Mwili ukipelekwa Kanisani
 Baada ya ibada Kanisani
 Hapa ni kuelekea maeneo ya makaburini

 Askari wakitoa heshima



 Muhongo na mke wake wakiweka shada la maua
 RPC akiwa shada la maua


 Muhongo akitoa shukrani

Post a Comment