0 Katika kuingia mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani,waumini wa dini ya kiislam katika Kijiji cha Kinesi wilayani Rorya,wamemshukuru mfanyabiashara na muumini wa dini hiyo Ramadhan Msomi Bwana,kwa kuwajengea msikiti na kupata mahala pa kufanya ibada katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu 

 Wakizungumza katika msikiti huo mara baada ya swala ya Ijumaa,wamesema jambo ambalo wamefanyiwa malipo yake atayafanya Mwenyezi Mungu kwa kuwa kwa sasa wameondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kufuata mahala pa kufanyia ibada
 Wamesema wapo wafanyabiashara wengi lakini Rama kwa kujenga Msikiti huo ameonyesha ni namna gani ambavyo aliiona changamoto ya usumbufu wa kufanya ibada na kuamua kuwajengea Msikitini.

 Waumini wakiwa kwenye swala ya Ijumaa msikiti mwa Rahman uliopo Kijiji cha Kinesi
 Ibada ikisimama ndani ya Msikiti wa Rahman

 Mawaidha baada ya SwalaPost a Comment