MKUU wa mkoa wa Mara,Dk.Charles Mlingwa,amewaponhgeza Waandishi wa Habari wa mkoa kwa ushirikiano wao wa karibu katika kuutangaza mkoa hususani katika fursa mbalimbali za uwekezaji likiwemo suala la viwanda ambapo kwa kusisitiza hilo katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari wamekuja na kauli mbiu isemayo""Sasa ni wakati wa Habari za uwekezaji katika Viwanda Mara" na kuguswa na kazi inayofanya Club ya Waandishi wa Habari mkoa wa Mara na kuamua kuichangia shilingi laki tano.
Meneja Uhusiano wa mgodi wa Acacia North Mara,Saimon Sanga,akizungumza namna mgodi huo unavyoshirikiana na Waandishi wa Habari ambapo pia walichangia kufanikisha maadhimisho hayo kufanyika vizuri zaidi
Wanahabari wakifatilia maadhimisho hayo
Mwenyekiti wa Mara Press Club(Mugini Jacob(kushoto)akiwa na mkuu wa mkoa wa Mara,Dk.Charles Mlingwa
Mwenyekiti akitoa taarifa ya Chama
Mwahabari George Marato(kulia) akibadilishana jambo na Katibu wa chama cha ACT-Wazalendo mkoa wa Mara,David Katikiro,kwenye maadhimisho hayo
Meneja wa Sido mkoa wa Mara,akizungumzia masuala ya viwanda kwenye maadhimisho hayo |
Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Mara,Boniphace Ndengo pia alipata fursa ya kuzungumza kwenye maadhimisho hayo
Kutoka mfuko wa PSPF-Meneja wa mkoa wa Mara,Deogratius Njuu,pia alizungumza na wanahabari na wadau waliohudhuria
Mwakilishi wa Azam Tv mkoa wa Mara,Augustine Mgendi,alitoa mawazo yake kwa viongozi wa serikali namna ya kuhakikishiwa ulinzi kwa Waandishi wa Habari
Mmoja wa Waandishi waliofanikiwa na kupata tuzo mbalimbali,Dinna Maningo,akizungumza namna anavyofanikiwa kwenye kazi zake za uandishi
msisitizo kutoka kwa mkuu wa mkoa
Picha ya pamoja ya Waandishi wa Habari wa mkoa wa Mara
Picha na wadau waliohudhuria maadhimisho hayo
Picha viongozi wa kamati ya utendaji ya Mara Press Club
Waandishi wakipata kumbukumbu
Masuala ya msosi pia yalihusika |
Post a Comment
0 comments