0
Na Shomari Binda
        Musoma,

Waandishi wa Habari hapa Nchini wameelezewa kuwa ni moja ya watetezi wa kubwa wa Haki za Binadamu katika Jamii kutokana na kazi wanayoifanya katika kutetea Haki mbalimbali za Binadamu wazohitaji kwa kuandika na kutangaza.

Kauli hiyo  ilitolewa na Mratibu wa Idara ya Mipango na Ujengaji Uwezo wa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto la ABC-Foundation,Andrea Migiro alipokuwa akizungumza na BLOG HII juu ya mpango wa kuanzisha chombo kimoja cha Utetezi wa Haki za Binadamu.

Alisema Waandishi wa Habari wamekuwa mstari wa mbele katika kupigania Haki za Binadamu kwa kuzitolea taarifa licha ya kufanya kazi katika mazingira magumu na wengine kuchukuliwa kutokana na taarifa wanazozitangaza na kuziandika.

Alidai Wanahabari bila uoga wamekuwa wakitumia vyombo vyaombo vyao kuelezea madhara yanayopatikana kutokana na kutokana na pale Haki za Binadamu zinapovunjwa zikiwemo za Wanawake na Watoto baadhi ya watu wanaoondikwa na kutangazwa kutokana na kuzivunja wamekuwa wakiwachukia Waandishi wa Habari.

Migiro alisema Shirika la ABC Foundation linawachukulia Waandishi wa Habari kama watu muhimu katika harakati za kupigania haki za Binadamu hivyo ni muhimu kutambua mchango wao wanaoutoa katika kufanya kazi hiyo.

Alisema katika chombo hicho cha Utetezi wa Haki za Binadamu cha pamoja kinachotarajiwa kuanzishwa kitakachoshirikisha Asasi na Taasisi mbalimbali Mkoani Mara,Waandishi wa Habari wanapaswa kuwemo na kufanya kazi kwa kushirikiana.

“Tumeshakaa kikao cha kwanza kwa kukutana na viongozi wa Asasi nyingine za kijamii zinazofanya kazi Mkoani Mara ambacho kiliratibiwa na CDR-Fund na kuna maazimio mbalimbali tuliyopanga kuanza nayo.

“Kuna madhara makubwa yanayowapata Watetezi wa Haki za Binadamu pamoja na Waandishi wa Habari,tunataka chombo hiki kufanya kazi kutokana na changamoto zinazopatikana tunataka chombo hiki kianzie hapa mkoani Mara na baadae kiwe cha Kitaifa,alisema Migiro

Post a Comment