0
Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Human Rights Watch, limesema kuwa serikali ya India imekosa kabisa kuwalinda watoto kutokana na dhulma za kimapenzi ambazo zinatendeka sana katika shule na taasisi za kuwatunza watoto.

Kwa mujibu wa shirika hilo, zaidi ya visa elfu saba vya ubakaji wa watoto huripotiwa kila mwaka , ingawa wataalamu wanaamini kuwa idadi kamili huenda ikawa juu kuliko inavyokadiriwa.

Watoto wanaoathiriwa na vitendo hivyo, mara kwa mara huteswa na kunyanyaswa na polisi.

Human Rights Watch limeitaka serikali kutilia mkazo sheria zilizopo na hata kufanyia mageuzi mfumo wa sheria ili kukabiliana na hali hii.

Ripoti hii inakuja wakati kuna kilio kikubwa kutoka kwa watu India hasa kuhusu ubakaji wa msichana wa chuo kikuu uliofanywa na wanaume watano na kusababisha kifo chake Disemba mwaka jana.

  Chanzo BBC NEWS

Post a Comment