0
MAKAHAMA ya hakimu mkazi wilaya ya Musoma mkoani Mara imemuhukumu kifungo cha maisha mkazi wa Nyamwaga wilayani Tarime Bw James Dotto kwa kosa la kuchoma nyumba moto.

Hukumu hiyo imetolewa hakimu wa Mahakama hiyo  Baraka Maganga ambapo amesema mahakama imethibitisha bila shaka mtumiwa huyo kutenda kosa  aprili 9 mwaka 2011 katika Kijiji cha Nyankanga Wilaya ya Musoma Vijijini.

Awali upande wa mashitaka umeileza Mahakama kuwa, mshitakiwa huyo alikuwa akiishi katika nyumba hiyo kwa muda mrefu na hakukuwa na ugomvi wowote ambao uliwahi kuushudia baina ya Dotto na Richard.

Mwendesha Mashitaka  wa jeshi  la polisi Aron Mihayo amesema kuwa hana kumbukumbu ya Makosa ya nyuma ya Mshitakiwa hivyo na kuiomba Mahakama kutoa adhabu kwa mujibu wa sheria.

 Kufutia maelezo hayo ya upande wa mashitaka na ushahidi ulitolewa mahakamani hapo,Mahakama imeona mshitakiwa ana hatia kwa mujibu wa kifungo cha 319 (a) ya sheria ya kanuni ya adhabu ya mwaka 2002 hivyo kumpa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani.

Kabla ya kutolewa kwa Hukumu hiyo mshitakiwa alitakiwa kujitetea mbele ya Mahakama kutokana na kosa lake na kudai kuwa hana cha kujitetea.

Hakimu Maganga amedai kuwa ametoa adhabu hiyo kwa mujibu wa sheria kutokana na kukithiri kwaMatukio ya uchomaji Nyumba ili iwe fundisho kwa watu wengine wanaofanya matukio kama hayo.

Post a Comment