CCM Mara yawakataa Wabunge A.Mashariki
-Nyerere amfuata
Bhanj kuanguka
-Akubali matokeo
na kukataa makundi
-Adai kama
yataendelea CCM isitegemee ushindi
Na Shomari Binda
Musoma,
Ni kama ambavyo unaweza kusema Chama cha Mapinduzi Mkoani Mara haina haja na
haiwataki Wabunge wa Afrika Mashariki baada ya kuwaangusha katika chaguzi
zinazoendelea ndani ya Chama hicho Nchi nzima katika nafasi mbalimbali za
uongozi.
Katika uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani mara wajumbe
wa mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa wiki wajumbe walimpigia kura ambazo
hazikutosha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho katika miaka mitano iliyopita
Charles Makongoro Nyerere ambaye pia ni Mbunge wa Afrika Mashariki na kumchagua
Christopher Sanya ambaye kisiasa ni mlezi wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Bunda.
Katika uchaguzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Shule ya
Wasichana ya Songe High School licha ya kuwashirikisha wagombea watatu katika
nafasi ya Mwenyekiti ushindani tangu mwanzo ulikuwa kwa
Makongoro Nyerere na
Christopher Sanya hali iliyopelekea kurudiwa kwa duru ya pili kwa wagombea hao
huku mgombea mwingine Mwenyekiti wa zamani wa Chama hicho Mkoani Mara Mwita
Chambiri akishindwa vibaya katika duru ya kwanza.
Blog hii iliwashuhudia wapambe na wapiga debe wa
kila mgombea wakihaha nje ya ukumbi wa mkutano huo kutafuta kura kwa wajumbe
huku kila upande ukionekana kumbana mwenzake asitumie matumizi ya fedha katika
kuwarubuni wajumbe huku baadhi ya wajumbe wakipasha kuwa hawa wanaangaika si
tulishakula chetu kuanzia jana (juzi).
“Sisi tumeshukula chetu tunachosubili ni muda wa kupiga kura
ufike tumalize kazi tumeshapewa maelekezo na hapa lazima tushinde maana kiasi
tulichopewa si haba na lazima tutashinda tumechoka,”alisikika mmoja wa wajumbe
akizungumza lakini hakuonyesha yupo kwa mgombea gani.
“Takukuru inabidi watafute njia nyingine mbadala ya
kudhibiti Rushwa naomba nikuhakikishie ngugu yangu lakini usitaje jina langu,
uchaguzi huu matumizi makubwa ya fedha yametumika na kuhakikishia hivyo nikiwa
kama mjumbe na tukiendelea hivi sijui kama tutafika kwa kumpata kiongozi chaguo
sahihi”,aliongea mmoja wa wajumbe aliyedai anatoka katika Wilaya ya Butiama.
Licha ya kuwepo na harakati za kutafuta kura kwa wapambe kwa
kupita huku na kule hali ya usalama ilihimalishwa katika uchaguzi huo kwa
kuwadhiti wale wasiokuwa wajumbe kuingia katika ukumbi wa mkutano wa uchaguzi
huku vitambulisho maalum vikitengenezwa kwa wale waliotakiwa kushuhudia
uchaguzi huo
Msimamizi wa uchaguzi huo Nazir Karamagi (MB) alimtangaza
Christopher Sanya majira ya saa sita usiku kuwa Mwenyekiti wa chama cha
Mapaindizi Mkoani Mara kwa kupata kura 481 na kumzidi Makongoro Nyerere
aliyepata kura 422 katika duru ya pili ya uchaguzi huo.
Katika matokeo ya awali yaliowahusisha wagomea watatu Mwita
Chambiri alipata kura 140,Charles Makongoro Nyerere alipata kura 371 huku
Christopher Sanya akipata kura 500 lakini hazikumuwezesha kushinda kutokana na
kutofikia asilimia 50.
Katika maneno yake ya shukrani Charles Makongoro Nyerere
alikubaliana na uwamuzi wa wajumbe kutokana na kura alizopata na kushindwa
kutosha na kutoa tahadhari ya kuepukana na makundi ambayo kama yataendelea
kuwepo katika Chama hicho katika chaguzi zinazo kuja kitapoteza Mitaa,Vijiji,Vitongoji
na Majimbo mengi.
“Mimi nimepitia katika kipindi kigumu sana cha miaka yangu mitano
ya uongozi sikutaka kupinda na nilikuwa imara na huenda ndio kimenigharimu na
leo,lakini hayo yamepita na namtaka mrithi wangu awe imara na asikubali
kuyumbishwa la sivyo miaka 5 ataiona
michungu kiuongozi.
“2014 na 2015 kuna uchaguzi wa Serikali za mitaa pamoja na
uchaguzi mkuu wa Mwaka 2015 bila kuwaunganisha hawa wajumbe kuwa wamoja na
kukusaidia katika masuala mbalimbali hakuna ushindi ambao utaweza
kupatikana katika chaguzi hizo,”alisema
Makongoro.
Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa Chama cha Mapinduzi (CCM)
Mkoani Mara Christopher Sanya alihaidi kuufanyia kazi ushauri uliotolewa na
mtangulizi wake ili yale yaliyomsukuma kuomba nafasi hiyo na kuaminiwa kupewa
yaweze kutekelezeka.
Sanya alisema atajitahidi kadri ya uwezo wake kuweza
kutokubaliana na kuyapa nafasi makundi katika kipindi chake cha uongozi na
kumpa nafasi kila Mwanachama kutoa maoni na ushauri wake katika kufanikisha
kile ambacho kinatarajiwa.
Charles Makongoro Nyerere
anaungana na Mbunge mwenzake wa Bunge la Afrika Mashariki Shy –Rozi Bhanj
kukataliwa na wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Mara baada ya Bhanj
kuangushwa na Agnes Marwa katika nafasi Mjumbe wa Baraza la Taifa (UWT) katika
uchaguzi wa Jumuiya hiyo Mkoani Mara.
Post a Comment
0 comments