0
BAADHI YA WACHEZAJI WA TIMU YA POLISI MARA WAKIWAFATILIA WENZAO WAKIWAJIBIKA MAZOEZINI


  Kikosi cha timu ya maafande wa Polisi Mara wamepania kuibuka na ushindi katika mchezo wao wa kwanza wa ligi daraja la kwanza Tanzania Bara dhidi ya Pamba ya Mwanza TP lindanda utakaopigwa kwenye dimba la CCM Kirumba oktoba 24 ikiwa ni safari ya kuelekea katika ligi kuu ya Vodaco katika msimu ujao.

Akizungumza na Blog hii katika mazoezi ya timu hiyo kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Karume Mjini Musoma,Mwenyekiti wa timu hiyo Inspekta Alon Mihayo amesema kutokana na mazoezi ambayo timu yake imeyafanya chini ya kocha mkuu wa timu hiyo Hafidh Salim akishirikiana na benchi la ufundi wanaamini watafanya vizuri na kupanda ligi kuu.

Amesema program zote ambazo kocha amekuwa akizihitaji zimefanyika kama ilivyotakiwa hivyo kilichobaki ni kusubili siku ifike ili waone kile walichopanda ila anaamini kwa hali waliyonayo wachezaji watafanya vizuri na kufikia malengo waliyopanga.

Mihayo amesema wamekuwa wapo karibu na wachezazi wote waliowasajili na kila mmoja kutekelezewa mahitaji yake na kudai kuwa watafanya kile ambacho wanatakiwa kukifanya ikiwa ni kuhakikisha wanashilikiana na uongozi ili kuweza kufanya vizuri kwenye ligi.

Mwenyekiti huyo wa kikosi cha maafande wa Polisi Mara ameongeza kuwa wanahitaji pia sapoti ya nashabiki na wadau wa timu hiyo katika mchezo wa ufunguzi jumatano ya octoba 24 katika dimba la kirumba hivyo yeyote atakaye weza kujisafirisha afanye hivyo ili kuweza kwenda kuitia nguvu timu katika mchezo huo muhimu.

Amesema iwapo watashinda katika mchezo huo utawaongezea hali ya kufanya vizuri katika mchezo wao wa pili octoba 27 dhidi ya Mwadui ya Shinyanga utakaofanyika katika uwanja wa Kambarage Mkoani humo

Post a Comment