0


Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Devotha Mwita (27) mkazi wa Kijiji cha Kitasakwa kata ya Bwiregi Wilayani Butiama amepigwa na kuumizwa vibaya na anayedaiwa kuwa ni mume wake baada ya kuchukua kisadolini ya mahindi na kisha kuipeleka Kanisani kama matoleo ya sadaka


 Akizungumzia tukio hilo katika Ofisi za Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Watoto la ABC Foundation zilizopo Mjini Musoma huku akibubujikwa na machozi,Mwanamke huyo alidai kuwa zaidi ya mwaka mmoja mume wake aliyemtaja kwa jina la Marato Mwita aliyezaa nae watoto wanne alimtelekeza na kwenda kuishi Jijijini Dar es salaam na kumuacha bila msaada wowote na kuamua kuokoka na kufanya shughuli za kilimo.

Alisema mume wake ambaye alirejea hivi karibuni kutoka Jijini Dar es salaam  alimpiga usiku wa januari 26 na kumuumiza sehemu mbalimbali za mwili wake na kumtegua mguu huku akizuia majirani kuja kumpa msaada wowote licha ya kukaa ndani kwa muda wa wiki moja kwa kushindwa kutembea.

Alidai baada ya kukaa ndani kwa wiki moja majirani waliamua kumpigia simu kaka yake ambaye alikuja kumuona na kumkuta mume wake ayupo na kuamua kumchukua kumpeleka katika hospitali ya Mkoa wa Mara kwa ajili ya kupatiwa matibabu baada ya kupitia polisi na kutoa taarifa.

"Kwa kweli nilipigwa na kuumizwa vibaya laiti kama ungeniona nilivyokuwa na kushindwa kutoka ndani ungenionea huruma,mimekaa ndani kwa wiki moja nikishindwa kutembea huku akishindwa kunihudumia hadi kaka yangu alipopewa taarifa na majirani na kuamua kunipeeka hospitali kwa ajili ya matibabu.

"Zaidi ya mwaka mmoja ameniacha bila msaada wowote mimi pamoja na wototo na mahindi ambayo yamepelekea mimi kupigwa baada ya kutoa Kanisani kama sadaka nimelima peke yangu na yeye amenikuta nimeshavuna kwa kweli imeniumiza sana na tangu huko nyuma amekuwa akininyanyasa na kunipiga mara kwa mara bila sababu za msingi,alielezea Devotha.

 Alisema baada ya kufanya shughuli za kilimo kwa kipindi chote huku akishiriki katika shughuli za Kanisa ambapo alisema kwa kiasi kikubwa viongozi wa Kanisa ndio waliompa imani kutokana na kuachwa na mume kwa muda mrefu huku akiwa na Watoto wake aliamua kutoa sehemu ya mavuno yake kwa ajili ya Kanisa.

Devotha alidai pale mungu akimsaidia na kupona majeraha aliyokuwa nayo atarajii kurudi kwa mume wake bali atafatilia kupata taraka na kuachana na maisha ya kunyanyasika na kufanyiowa ukatili mara kwa mara na kuendelea kuishi maisha ya kinyonge.

Akizungumzia namna matukio ya Ukatili kwa Wanawake yanavyoendelea katika Jamii,Mratibu wa Idara ya Mipango wa Shirika la Kutetea Wanawake na Watoto la ABC Foundation,Andrea Migiro alisema Jamii bado inahitaji mabadiliko makubwa katika kuhakikisha matukio ya Ukatili dhidi ya Wanawake yanakomeshwa.

Alisema Mwanamke bado anaendelea kuishi maisha ya kinyonge na kunyanyaswa katika baadhi ya familia na hivyo kukwamisha nguvu kazi na kujiongezea kipato katika familia lakini pia akiendelea kuwa mtu wa chini na dhaifu katika Jamii.

Migiro alisema Ukatili wa Kijinsia unakuwa na athari nyingi kwa Jamii ikiwa ni pamoja na athari za kisaikolojia kama mfadhaiko,huzuni,majonzi,hofu,aibu,kutengwa na Jamii na kupoteza heshima vitu ambavyo vinamfanya mhanga wa Ukatili kushindwa kufanya shughuli za kila siku za kujiongezea kipato.

Alisema Shirika la ABC Foundation moja ya mipango yake kwa mwaka 2013 kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ni kutoa elimu ya kutosha kuhusiana na athari dhidi ya Ukatili katika Jamii ili kuweza kutokomeza matukio hayo na Jamii kubadilika na kumuona kila mmoja ana nafasi yake katika familia.

Post a Comment