0
Redd's Miss Sinza 2013, Prisca Element (katikati) akiwa na Mshindi wa pili Happynes Maira (kulia) na Mshindi wa tatu, Sarahy Paul, akipunga mkono kwa furaha mara baada ya kutangazwa kutwaa Taji hilo lililokuwa likishikiliwa na Redd's Miss Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigit Alfred. 

Shindano hilo lililokuwa la aina yake na ushindani wa nguvu limemalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa Meeda Club, huku mashabiki wa fani ya urembo walioshuhudia shindano hilo wakisebeneka na burudani kutoka kwa bendi ya African Stars Twanga Pepeta. 
Nafasi ya Nne ilichukuliwa na Mrembo Nicole Michael na nafasi ya Tano ikitwaliwa na Nasra Hassan. 

 

Post a Comment