0

VIONGOZI na watumishi katika Idara za Serikali za Mitaa wametakiwa kufanya kazi kwa kuwajibika na kuhakikisha inawatumikia wananchi kwa kuwa ngazi ya Serikali za mitaa ina wajibu wa moja kwa moja kufanya hivyo.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa mkoa wa Mara Gabriel Tuppa katika maazimisho ya sherehe za Serikali za Mitaa ambazo kimkoa zilifanyika katika uwanja wa sabasaba Mjini Tarme.

Alisema viongozi wengi wamekosa uwajibikaji katika majukumu yao ya kila siku na wengine kufanya kazi kwa mazoe na masrahiyao binafsi bilakuzingatia wanapaswa kuwatumikia Wananchi ambao ndio wenye mamlaka katika Serikali za mitaa.

Tuppa alisema Viongozi na watendaji katika ngazi ya Serikali za mitaa wanapaswa kuzingatia wajibu na sheria za utumishi ili kuweza kuwatumikia Wananchi na kujenga utamaduni wa kutoa taarifa ya mapato na matumizi kwa Wananchi.

"Shida kubwa katika ngazi ya Serikali za Mitaa ni kushindwa kwa viongozi na watendaji  kushindwa kutoa taarifa ya mapato na matumizi kwa Wananchi kwa muda mrefu hali ambayo inapelekea kukosa imani nanyi.

"Nawahimiza Viongozi wote pamoja na watendaji katika ngazi ya Serikali za mitaa kuzingata wajibu wenu katika uwajibikaji na hasa kutoa taarifa ya apato na matumizi pamoja na kusimamia fedha zote zinazokuja katika mamlaka zenu.

"Si vyema kufuja fedha za Umma ambazo zinakuja katika mamlaka zenu kwa lengo la shughuli mbalimbali za Wananchi ambazo zimekusudiwa na muache kujihusisha na vitendo vya rushwa ili muwasaidie Wananchi,alisema Tuppa.

Alisema vitendo vya baadhi ya viongozi wasio waaminifu kujiingiza katika vitendo vya rushwa ili waweze kutoa msaada kunawafanya Wananchi kuichukia Serikali yao  kutokana na vitendo hivyo.

Mkuu huyo wa mkoa wa Mara aliwataka Wananchi kutambua Serikali za Mitaa ni zao hivyo kujenga utaratibu wa kushiriki katika mikotano inayohitishwa katika maeneo yao na kuacha watu wachache kushiriki na kupitisha mazimio ambayo baadae yanakuja kulalamikiwa.
Post a Comment