WARSHA INAYOENDESHWA NA SHIRIKA LA WANAWAKE KATIKA MAENDELEO AFRIKA(WILDAF) KATIKA UKUMBI WA FARAJA MJINI MUSOMA
VIONGOZI wa makundi na Asasi mbalimbali katika jamii yanayojihusisha
na utetezi wa Haki za Wanawake wametakiwa kutumia mafunzo
wanayoyapata katika warsha kuielimisha jamii inayowazunguka ili kila
mmoja aweze kuelewa athari zinazopatikana kutokana na kuvunjwa kwa
haki zikiwemo za Wanawake.
Kauli hiya ilitolewa na Afisa Mipango na Mafunzo wa Shirika la
Wanawake katika Maendeleo Afrika(WILDAF) Anlico Sengo katika ufunguzi
wa warsha ya kuongeza uwezo kwa makundi ya Wanawake juu ya Haki ya
Wanawake Kimataifa,Afrika na Sheria ya Ndoa inayofanyika kwa siku tatu
katika ukumbi wa jengo la faraja mjini Musoma.
Alisema mafunzo yanayotolewa kuhusu Mwanamke kuelewa Haki zake
hayawezi kumfikia kila mmoja kwa kushiriki warsha bali wale
wanayoyapata wanalo jukumu la kuhakikisha wanayashusha kwenye jamii na
sio kushiriki na kushindwa kuyafanyia kazi inayo kusudiwa.
Afisa huyo alisema katika muda wa siku tatu yatatolewa mafunzo ya
Mkataba wa kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya Wanawake uliosainiwa
mwaka 1979 na kudai mambo watakayojifunzo kwenye mkataba huo yanapaswa
kwenda kuifahamisha jamii ili nayo iweze kuuelewa mkataba huo.
Alisema kabla ya kuwa na mkataba ulimwengu ulianza harakati za
kutambua Haki za Binadamu bila kujali hali zao za kijinsia ya kuweka
tofauti kati ya Mwanamke au Mwanaume kila wakati wanaharati
ambalimbali wamekuwa wakipigania juu ya kuzitambua haki.
Anlico alidai ni muhimu kuzingatia mikataba mbalimbali na harakati za
Wanawake katika mikutano ya Kimataifa ukiwemo mkutano wa Kimataifa wa
Wanawake wa Mexico wa mwaka 1975,mkutano wa Denmark wa mwaka
1980,mkutano wa Kenya wa mwaka 1981 na mkuatano wa Kimataifa wa
Wanawake wa Beijing China wa mwaka 1995.
Akizungumzia Haki ya mali katika ndoa,mkufunzi wa warsha hiyo Desteria
Haule alisema Sheria ya ndoa imeainisha Haki ya kuwa na mali kati ya
wanandoa katika kumiliki mali binafsi kama vile gari,shamba au nyumba
na hata inapotokea ndoa kuvunjika mali binafsi haita husika katika
mgao na kudai wapo Wanawake ambao pia umiliki mali laki hawajui haki
zao.
Alisema mali zinazogawanywa ni zile zinazopatikana kwa juhudi za
pamoja kati ya wanandoa na haijalishi kama Mwanamke alikuwa hana kazi
za kuingiza kipato kwani Mahakama ilishatoa msimamo kuwa kazi zote za
nyumbani zinazofanywa na Mwanamke zinahesabika ni mchango mkubwa wa
upatikanaji wa mali za ndoa.
Kwa upande wa washiriki wa warsha hiyo walisema kutokana na umuhimu wa
mafunzo hayo watayazingatia na kuahidi kuyazingatia na kupeleka ujumbe
kwa jamii ili kila mmoja aweze kuelewa haki pamoja na mikataba
mbalimbali ambayo inamzungumzia Mwanamke juu ya Haki.
Post a Comment
0 comments