0
JESHI la polisi mkoani Mara limetangaza kutoa kiasi cha shilingi milioni 1 kwa mtu yoyote atakayefanikisha kutoa taarifa na kukamatwa kwa watu wanaojihusisha na matukio ya mauaji ya Wanawake wilayani Butiama.

Ahadi hiyo imekuja kutoka ndani ya jeshi hilo kufuatia kuendelea kutokea kwa vitendo vya matukio ya mauaji dhidi ya Wanawake yanayokuwa yakitokea mara kwa mara hususani wilayani humo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake mara baada ya kutokea kifo cha Anastazia Shore Kijiji cha Kwibara,kamanda wa jeshi la polisi mkoani Mara Ferdnand Mtui alidai kinachokwamisha kupata taarifa za wauaji ni kucheleweshwa kwa taarifa.

Post a Comment