AFISA MFAWIDHI WA MFUKO WA JAMII WA PSPF MKOA WA MARA SUDI HAMZA AKITOA ELIMU KATIKA MOJA YA SHUGHULI ZA MFUKO HUO MJINI MUSOMA
MFUKO
wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) umewataadhalisha wastafu kujiepusha ujumbe
wa simu wanaotumiwa kuhusiana na michango yao na kuwataka kutuma fedha
ili waweze kurekebishiwa kile kinachodaiwa kuwa ni mapunjo.
Tahadhari
hiyo ilitolewa kwa nyakati tofauti na Afisa Mfawidhi wa PSPF mkoani
Mara Sudi Hamza wakati akizungumza na wafanyakazi wa idara mbalimbali za
Serikali na watu binafsi kuhusu umuhimu wa kujiunga na mfuko wa
uchangiaji wa
hiari(PSS).
Sudi alisema hakuna ujumbe wa namna hiyo unaotumwa kutoka PSPF na tayari makao makuu umeshatoa taarifa kwa vyombo vya habari hivyo wasikubaliane na ujumbe unaotumwa.
Alisema tayari alishapokea taarifa kuhusiana na kutumwa kwa ujumbe huo na kuwasisitizia wastafu iwapo watapokea ujumbe wa namna hiyo kuwasiliana ofisi za PSPF Mara ama kumpigia simu yake ya mkononi ambayo wanachama wengi tayari alishawapatia.
Akizungumzia fursa zilizopo katika mfuko wa uchangiaji wa hiari(PSS)alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa benki ya NMB tawi la Musoma,Sudi alisema fao la elimu pamoja na ujasiliamali ni moja ya fursa zinazotolewa kwa wanachama kupitia uchangiaji wa hiari.
Sudi alidai masuala ya elimu ni jambo la msingi hivyo PSPF imeliingiza kama fao kwa wachangiaji wa hiari ili zinapopatikana fursa za kusoma mwanachama asipate kikwazo katika kutafuta elimu.
Alisema PSPF inaendelea kuhamasisha kila idara pamoja na wajasiliamali na umuhimu wa uchangiaji wa hiari na kudai licha ya mafao ya elimu na ujasiliamali hata mchangiaji wa hiari kama wanac hama wengine anaruhusiwa kupata mkopo wa nyumba kama wengine.
Aidha Afisa huyo wa PSPF mkoa wa Mara akiwa katika chuo cha ualimu Musoma Utalii alitoa zawadi ya shilingi laki 7 kwa wanafunzi na walimu wa ualimu waliotajwa kufanya vizuri katika ufundishaji na ufaulu na kusisitiza wataendelea kutoa motisha kwa watakaofanya vizuri katika maeneo yao ya majukumu.
Post a Comment
0 comments