JESHI
la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) limelaani vikali askari wake
aliyesababisha fujo na kupelekea kupigana kati ya askari polisi na
askari wa jeshi hilo katika kituo cha polisi mjini Tarime.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Musoma kwa
niaba ya Mkuu wa Majeshi ya Nchi Kavu,Mkuu wa Bregedia 202 kundi la Vikosi,Brededia
Jenarali Methiw Sukambi alisema askari huyo amekiua kiapo chake hivyo hastahili
kuendelea kuitwa mwanajeshi wa JWTZ.
Alisema kitendo hicho kimefanywa na askari binafsi na
siyo jeshi na kudai taratibu za jeshi zinafundisha na kuelekeza Afisa na askari
kuwa mtiifu na mwenye nidhamu na anatakiwa kutii mamlaka na kufuata sharia za
nchi kwa mujibu wa Katiba.
Brededia jenarali Sukambi,alisema jeshi la wananchi
linalaani kitendo cha askari huyo pamoja na wengine walioshiriki katika tukio
hilo aliloliita la aibu kubwa kwa vyombo vya dolakupigana hadharani kama
ilivyotokea.
“Nimeagiza sheria na taratibu zichukuliwe dhidi yake
na kwa wale wenzake walioshiriki kwa namna moja ama nyingine na nichukue nafasi
hii kutoa pole kwa wale waliopata madhara kutokana na vurugu hizo.
“Natoa wito kwa wanajeshi wote kuzingatia viapo vyao,kutii sheria na taratibu za nchi pamoja na kutii mamlaka za kiraia kwa
mujibu wa Katiba ya Tanzania,”alisema.
Alisema wamefanya mazungumzo na viongozi wa mkoa na
wilaya na kwa pamoja wamekubaliana kufanya kazi kwa pamoja na kuendelea
kushirikiana kudumiha ulinzi na usalama wan chi na kuwapongeza wananchi
waliotoa taarifa kuhusiana na tukio hilo na hivyo kuzuia madhara makubwa zaidi
ambayo yangeweza kutokea.
Post a Comment
0 comments