KATIKA kuendeleza michezo Manispaa
ya Musoma,Mjumbe wa Halimashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi(CCM)wilayani Musoma,Vedastus
Mathayo,ameialika timu ya vijana ya Azam FC kucheza michezo miwili ya kirafiki
na kombani ya vijana wa Musoma.
Akizungumzia kuhusiana na kualikwa
kwa timu hiyo,mratibu wa mashindano ya kukuza vipaji ya Mathayo Cup
yanayofanyika kila mwaka mjini Musoma,Amani Richard,amesema muandaaji wa
mashindano hayo amekusudia kuleta mabadiliko ya soka Manispaa ya Musoma na mkoa
wa Mara kwa ujumla na kuahidi kuzialika timu mbalimbali kwaajili ya changamoto
za michezo.
Amesema Mathayo amekubali
kugharamikia malazi na chakula na huduma nyingine kwa timu ya vijana ya Azam
kwa siku 2 itakazokuwa Musoma na tayari wamekwesha watumia barua uongozi wa
timu hiyo na wanachokisubilia ni majibu kutoka kwa timu hiyo.
Amani amesema timu ya kombaini ya
Musoma imepatikanakutoka kwenye mashindano ya mwaka huu yanayofikia tamati
desemba 10 kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Karume mjini hapa ambapo jumla ya
timu kutoka Kata 13 za Manispaa ya Musoma zimeshiriki na kupatikana vipaji
vingi vya vijana.
“Tunashukuru kwa fursa hii nzuri
ambayo tumeipata kutoka kwa muaandaaji wa mashindano ya Mathayo Cup kwa
kuialika timu ya vijana ya Azam FC kwa kuwa ni fursa nzuri kwa vijana wa Musoma
kuweza kuonyesha vipaji vyao.
“Tayari tumeshatuma barua kwa
uongozi wa timu ya Azam FC na tunaamini kwa kuwa ni watu wa michrzo na
wanaofanya jitihada katika kuendelea soka hususani soka la vijana watatukubalia
ombi letu na kuhakikisha timu yao inafika Musoma na kucheza michezo hiyo ya
kirafiki,alisema Amani”.
Amesema katika barua yao wameiomba
timu hiyo kucheza michezo 2 kwenye uwanja wa Karume kati ya desemba 13 na 14 na
tayari wakazi wa Manispaa wameshakuwa na hamu ya kuiona timu ya vijana ya Azam
ikicheza na kombaini ya Musoma.
Akizungumzia mualiko huo kwa njia ya
simu,Meneja wa timu ya Vijana ya Azam FC Philipo Alando amesema wamepokea
barua kutoka kwa mratibu wa mashindano ya Mathayo Cup yanayofanyika Musoma kwa
lengo la kucheza michezo hiyo ya kirafiki na jibu kamili na jibu kamili
linatarajiwa kutolewa wakati wowote na uongozi wa Azam.
Post a Comment
0 comments