WACHUNGAJI
wa madhebu ya Dini katika wilaya ya Musoma mjini,wamewakemea viongozi wa vyama
vya siasa wanaopanda kwenye majukwaa na kugomesha michango ya maendeleo.
Wakizungumza
katika mkutano wa wadau wa elimu uliohitishwa na Mkuu wa Wilaya ya
Musoma,Jackson Msome,katika ukumbi wa uwekezaji wa mkoa wa Mara,viongozi hao
walisema sio jambo la busara kuwahamasisha wananchi kuacha kuchangia maendeleo
yao hususani sekta ya elimu.
Waliema
kwenye maeneo mengine ya nchi,wananchi wamekuwa mstari wambele kuchangia maendeleo
yao na kupata mafanikio lakini kwa Musoma hali imekuwa tofauti huku viongozi wa
kisiasa wakiwa mbele kuwagomesha wananchi wasichangie.
Mchungaji wa
Kanisa la Evangelistic Asemblius of God(EAGT) Moses Sephania, alisema siasa
isiweze kuwafanya watu kuacha masuala ya msingi na kuahamasika kuacha kuchangia
ujenzi wa maabara mashuleni jambo ambalo litapelekea kuzalisha wanafunzi
wasioweza kuendelea na masomo ya juu.
Alisema
suala la maabara ni jambo la msingi katika maendeleo ya elimu na kama kuna
mwanasisa anayepanda kwenye majukwaa na kutoa maneno ya kugomesha kuchangia
atoe sababu za msingi za kutokufanya hivyo.
Kwa upande wake,Askofu wa Kanisa la New Life
Church,Daniel Ouma Dawa,alisema anachoweza kukifanya na kuwakemea kwa nguvu za
Mungu wale wote wanaogomesha michango ya maendeleo kwa kuwa sio watu wema
katika Wilaya ya Musoma.
“Kwa jina la
Yesu,watu hawa washindwe na kuwaacha wananchi huru ili waweze kuchangia
maendeleo yao ya elimu na kuweza kujikomboa katika soko la ajira,sisi
hatutachoka kuhamasisha katika nyumba za ibada ili kutambua umuhimu wa
kuchangia elimu,”alisema Askofu Dawa.
Awali
akifungua mkutano huo uliowashirikisha watu wa kada mbalimbali na wadau wa
elimu,Mkuu wa Wilaya ya Musoma,Jackson Msome,alisema wanaendelea kutekeleza
agizo la Rais Kikwete juu ya ujenzi wa maabara lakini kuna wanasiasa
wanaowapotosha wananchi na kuwakataza kuchangia.
Alisema
kuanzia sasa ametoa agizo katika vyombo vya dola juu ya kuwashughulikia wale
wote wanaopotosha suala la ujenzi wa maabara kwa kuwa wanaendelea kuwarudisha
nyuma wananchi juu ya kujiletea maendeleo.
Mkuu huyo wa
Wilaya alisema ujenzi wa maabara umefikia asilimia 60 na kuwataka watendaji
kuendelea na uhamasishaji wananchui juu ya umuhimu wa kuchangia na kujiepusha
na maneno ya wanasiasa wanayoongea majukwaani.
Post a Comment
0 comments