0

 VIJANA WALIJITOKEZA KUPOKEA JENEZA KAMA INAVYOONEKANA

  ASKARI POLISI NAO WALIJUMUIKA KUPOKEA MWILIWA MWENZAO ALIYEAMUA KUJIUA KWA KUJIPIGA RISASI MDOMONI HUKO MANYONI MKOA WA SINGIDA FEB,2,2015

 JENEZA LINAONGIZWA NDANI YA BANDA LILILOANDALIWA NA MAITI YAKE HAIKUINGIZWA NDANI YA NYUMBA KWA KILE KILICHODAIWA KUWA NI MKOSI.
 NDUGU WAKILIA AKWA UCHUNGU WAKATI MARA BAADA YA MWILI KUWASILI
 JENEZA LIKITELEMSHWA NDANI YA KABURI KWA AJILI YA MAZISHI
 WANASHUSHA TARATIBU



 WANASHUSHA CHINI ILI KURUHUSU HATUA YA KUZIKA


 PADRI ALOIS  MAGABE ANATOA NASAHA ZA MWISHO HUKU AKISISITIZA WATU WANAOJIUA KANISA HALINA NAFASI YA KUENDESHA IBADA YA MAZISHI

 
Aliyekuwa askari wa jeshi la polisi hapa nchini namba G 4228PC Aloyce amezikwa nyumbani kwao wilayani Serengeti huku akishindwa kuzikwa kwa heshima za kijeshi wala kuombewa dua na kiongozi wa dini.

Ilidaiwa na baadhi ya watu walioshuhudia maziko hayo,askari huyo alishindwa kuzikwa kijeshi kutokana na kuonyesha uoga huku viongozi wa dini wakidai mtu aliyejiua si vyema kuombewa dua.

Awali taarifa zilidai askari huyo mnamo tarehe 02/02/2015 majira ya saa 10.35hrs ambaye alikuwa dereva wa OCD-MANYONI alifika kwa “armoury keeper” na kumuomba amkabidhi silaha kwani anasafari na OCD,alikabidhiwa silaha aina ya SAR NO.10065077ikiwa na risasi kumi.

Aliondoka na silaha hiyo na kuingia ndani kwake ambapo ni karibu sana na armoury na kuingia ndani ambapo aliingiza mtutu wa silaha hiyo mdomoni na kujipiga risasi huku akiwa amelala kitandani na kufariki hapo hapo.

Marehemu ameacha ujumbe kuwa ameamua kujiua mwenyewe kwa ridhaa yake na asilaimiwe mtu yeyote kuhusiana na kifo chake.mwili wa marehemu umehifadhiwa mortuary manyoni gvt hospital kwa ajili ya uchunguzi.

Pia katika ujumbe wake amedai mwili wake upelekwe kwao na S/SGT.MARWA NA SGT.MTAKI wa Polisi Singida.

Post a Comment