0
   MTOTO ANASULIKA KIFO BAADA YA KUTUPWA CHOONI.

         Na-Shomari Binda
            Musoma.

Mtoto wa kike anayekadiliwa kuwa na umri wa mwaka mmoja na nusu amenusulika kifo baada ya kutopwa katika shimo la choo na kuokolewa na wasamalia wema.

Tukio la kutupwa kwa mtoto huyo lilibainika leo asubuhi katika mtaa wa bandarini kata ya iringo katika manispaa ya Musoma.

Akizungumza na blog hii mmoja wa shuhuda wa tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la mama Torry alisema kuwa alisikia kilio cha mtoto kikitokea katika shimo la choo alipokuwa akifanya usafi majira ya saa 12 asubuhi na ndipo alipoamua kuwajulisha majirani kwa ajili ya msaada zaidi.

Shuhuda huyo aliongeza kuwa baada ya majirani kufika walifanya jitihada za kubomoa mfuniko wa shimo la choo hicho na kufanikiwa kumtoa mtomto huyo akiwa mzima.

Kwa upande wake Hamisi Bobera ambye pia alishuhudia tukio hilo alisema kuwa nusura ya mtoto huyo ilipatikana baada ya choo hicho kuanza kutumika hivi karibuni licha ya kuwa na kina kirefu.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Mara kamishina msaidizi wa jeshi la polisi Robert Boaz alisema kuwa wananchi watakaokuwa wanatambua mama au mlezi ambaye alikikuwa na mtotot na kwa sasa hayupo nae kutoa taarifa polisi au serikali za mtaa ili waweze kumbaini aliyehusika na tukio hilo.

Kamanda boazi alisema mtoto huyo kwa sasa amekabidhiwa katika timu ya ulinzi wa mtoto ya manispaa ili aweze kutafutiwa hifadhi huku jitihada za kumtafuta aliyefanya kitendo hicho zikiendelea.

Wakati huo huo kamanda wa polisi mkoani Mara alisema kuwa mtu  mmoja mwanaume ameokotwa akiwa amekufa na kuaribika katika kijiji cha kenyamota wilayani Serengeti na kushindwa kutambulika.

Alisema kuwa mtu huyo alikuwa amevaa suruali ya langi ya udongo na shati nyeupe yenye  ufito mwekundu kifuani na kuwataka wananchi ambaye wanaweza kuhusiana na mtu huyo kuwasiliana na jeshi la polisi ili kufanya uchunguzi zaidi wa kifo cha mtu huyo.
 

Post a Comment