0
                     CHAKULA CHA MSAADA CHAZUA GUMZO BARAZA LA MADIWANI

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Musoma vijijini Dk. Kalaine Kunei amesema kuwa suala la ucheleweshwaji wa Mahindi ya chakula cha msaada ni la Kitaifa na si mzabuni aliepewa tenda ya kusambaza mahindi hayo.

Hayo ameyasema leo katika kikao cha baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbu wa mikutano wa Halmashauri hiyo.

Amesema kumekuwa na upungufu katika ghala la Taifa la chakula Mkoani Shinyanga kutokana na kuhudumia mikoa ya Kanda ya Ziwa hali ilipelekea kuwepo na foleni ya Magari Mkoani humo inayosubiri kupatikia mahindi hayo.

Dr. Kunei amesema kuwa baadhi ya Kata katika Halmashauri hiyo ya Musoma zimekwisha pata Mahindi hayo na zile ambazo bado hazijapata zinaendelea kushughulikiwa.

Awali Diwani wa Kata ya Nyamimange Nyaswe Chacha alihoji kitendo cha baadhi ya Kata kupewa mgawo wa mahindi mara mbili wakati Kata nyingine zikiwa bado hazijapata hali iliyopelekea baadhi ya madiwani wengine kulizungumzia suala hilo.

Akizungumzia suala la Elimu Katibu tawala wa Halmashauri ya wilaya ya Musoma Bi. Debora Makinga ameomba madiwani wa Halmashauri hiyo kusimamia ujenzi wa vyumba vya madarasa vilivyobaki ili kila mwanafunzi aliefaulu kwenda Sekondari aweze kupata nafasi hiyo.

Post a Comment