0
        POLISI MARA BINGWA LIGI YA WILAYA

Timu ya maafande wa polisi Mara wametangazwa kuwa mabingwa wa ligi ya taifa ngazi ya wilaya ya Musoma baada kumaliza ligi hiyo kwa kufikisha pointi 30 kutoka na michezo 10 waliyoshuka dimbani.

Polisi Mara ambayo kwa mwaka huu imepania kufika mbali imeanza kuonyesha dhamila yao katika ligi ya wilaya iliyomalizika katika uwanja wa kumbukumbu ya karume mjini hapa baada ya kuzifunga timu zote zilizoshiriki katika ligi hiyo.

Akitoa vyeti vya ushiriki kwa timu zilizoshiriki ligi hiyo mwenyekiti wa chama cha soka manispaa ya Musoma(FAMT)Dedid Sungura alizitaka timu zote zilizopata kushiriki ligi ya taifa ngazi ya mkoa wa Mara itakayoanza hivi karibuni kujipanga na kufanya maandalizi mazuri ili ziweze kufanya vuzuri katika ligi hiyo.

Sungura amwezitaka timu za polisi,kigera fc na Musoma shoting kufanya usajili makini na kuwashirikisha wanachama wao na wadau wengine ili kuwaongezea nguvu ya kufanya maandalizi kabla ya kuanza kwa ligi ya mkoa.

Kwa upande wake msemaji wa timu ya polisi Mara Musa Masoud(keita)akizungumza na Tanzania daima alisema kuwa baada ya kutwaa ubingwa wa ligi ya Taifa ngazi ya wilaya sasa nguvu zao wamezielekeza katika ligi ya mkoa ili kuweza kupata nafasi ya kushiriki ligi ya Taifa ngazi ya Taifa.

Keita alisema kuwa wamedhamilia kwa msimu huu kufanya vizuri katika hatua mbalimbali baada ya kupata ushirikiano kutoka kwa kamanda wa polisi mkoani Mara Robart Boaz na wadau wengine wa timu hiyo na kuwataka wachezaji wengine wanaotaka kujiunga na timu hiyo wafike katika mazoezi yatakayoanza hivi karibuni baada ya mapumziko ya kumalizika kwa ligi ya wilaya.

Post a Comment