0
WANA CCM

MWANDISHI WA HABARI "KULA SHAVU" UJUMBE WA MKUTANO MKUU WA TAIFA CCM
 
-Katibu wa CCM atoa onyo kali kwa watakaopiga kampeni
 
-Asema rushwa ni adui wa haki wawaache wanachama wawachague kutokana na uwezo wao.

 
Butiama

JINA la Mwandishi wa habari wa gazeti la Uhuru na Mzalendo Wilaya ya Musoma Mkoa wa Mara Eva-Sweet Musiba limeteuliwa kuwa miongoni mwa wagombea nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake , Katibu wa CCM Wilaya ya Butiama, Mercy Mollel alisema kuwa majina hayo yamepitishwa na ngazi ya Mkoa huku yakisubiri uchaguzi katika mkutano Mkuu wa CCM wilaya hiyo ambao utafanyika septemba 29 mwaka huu.

Alisema kuwa zoezi la uchukuaji na urudishaji wa fomu ulishafanyika kwa mafanikio makubwa ambapo wanachama wengi walijitokeza kuchukua fomu ili kuwania nafasi mbalimbali katika chama hicho.

Alisema kuwa taarifa hiyo ya kutangaza majina ya wagombea ni wao kujijua kuwa wameteuliwa lakini si ruhusa kupiga kampeni hadi pale watati utakapofika wa kupigiwa kura kwenye ukumbi wa mikutano wa CCM mkoa huo.

Mollel alitoa onyo kali kwa mgombea yeyote atakayepiga kampeni kwa wanachama kwani akigundulika hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya mgombea huo.

Alitoa wito kwa wagombea hao kufuata kanuni na taratibu za uchaguzi na kuwaacha wanachama kuwachagua kutokana na uwezo wao na sio fedha kwani katiba ya chama hicho.

“Katiba yetu inasema kuwa sitopokea wala kutoa rushwa hivyo natoa wito kwa wagombea wote wa nafasi mbalimbali waache wanachama wawachague kutokana na uwezo wao sio kutumia fedha zao kwa kutoa rushwa,”alisema Mollel.

Mollel alizitaja nafasi zilizotolewa ambazo zinawaniwa ni pamoja na Katibu wa siasa na uwenezi na majina yaliyorudi ni Bwire Gibuma, Ntobi Ntobi, Japhet Werema, Nafasi ya Katibu wa uchumi na fedha ni Baraka Imani, Aron Mnema, Magina Nyauko, Nafasi ya Wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya kundi la Wanawake ni Tabitha Idd, Wegesa Witimu, Mwajuma Magoti na Bhoke Ngurube.

Nafasi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa ni Wegesa Witimu, Break Chisumo, Yohana Mnema, Rudia Mazera, Nestor Matiko na Happiness Masagara. Nafasi ya kundi la wazazi ni Fidelis Igonge, Wambura Kishamuri, Heonyo M. Heonyo, John Nyamisana, Ibrahim Makanya na Jemsi Matongo.

Nafasi nyingine ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa ni Nyaget Adam, Joseph Chief, Brasius Chuma, Fidelis Igonge, Gerald Kasonyi, Sebastian Makakila, Rashid Makka, Jerome Massawe, Eva-Sweet Musiba wengine ni Vivian Juma, Nyabukika B. Nyabukika, Magige Nyerere, Bhoke Ngurube, Rosemary Olinda na Wegesa Witimu.

Alisema kuwa nafasi ya Halmashauri Kuu vijana haikuweza kutoa wateuliwa kwa kuwa walioomba wote walikuwa na umri mkubwa hivyo kukosa sifa lakini tayari wameshazitangaza upya na watu wameshachukukua fomu na wiki mbili zijazo majina yatatolewa.

Aliongeza kuwa kwa sasa wanasubiria majina ya Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo na wajumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa kupitia Wilaya wanasubiria kutoka katika kikao cha Halmashauri kuu CCM Taifa

Post a Comment