0
MBUNGE WA VITI MAALUM KUPITIA VIJANA CCM MKOA WA MARA ESTER BULAYA AKIWA KATIKA MOJA YA MASHINDANO ANAYOANDAA,HAPA ILIKUWA BUNDA

MSISITIZO LAZIMA KUPEANA VIJANA

NIKO NA YUSUF MAGASHI WA REDIO FREE AFRIKA TUKICHUKUA DATA

NOTI KWA MABINGWA NIZAKUFIKIA

TOWN STARS FC AMA WAPIGA DEBE NDIO WALIKUWA MABINGWA WA BUNDA ESTER BULAYA CUP 2012

IKAJA ZAMU YA MANISPAA YA MUSOMA KABLA YA KUPEANA VIFAA WATU WANAPEWA MANENO

KATIBU WA VIJANA WA CCM WILAYA YA MUSOMA KING AKITOA MAELEZO HUKU VIFAA VYA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI NNE VIKIWA MEZANI

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA VIJANA WA CCM KATA YA MWIGOBERO ALIYEMALIZA MUDA WAKE ELIAS KERENGE AKIPOKEA VIFAA VYA KATA HIYO AMBAPO KATA ZOTE 13 ZA MANISPAA YA MUSOMA WALIPATA VIFAA VYA MICHEZO
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mara kupitia vijana (CCM) hivi karibuni anatarajiwa kuendelea na harakati  zake za kugawa vifaa vya michezo katika Wilaya za Mkoa wa Mara ikiwa na lengo la kufanyika kwa mashindano kwa vijana katika kuibua vipaji na kujipatia ajira kupitia michezo.

Safari hii kwa taarifa ambazo Blogu hii imezipata Mbunge huyo anatarajiwa kutoa vifaa katika Wilaya mpya ya Butiama ikiwa zoezi kama hilo sanjari na mashindano likiwa limefanyika katika Wilaya za Serengeti,Bunda na Musoma mjini.

Akizungumza wakati akifunga mashindano ya Ester Bulaya Cup katika Wilaya ya Bunda Mbunge huyo ambaye amepania kutimiza azima yake ya michezo kwa Vijana alihaidi kuhakikisha kila Wilaya katika Mkoa wa Mara inapata vifaa na kufanya michezo mara kwa mara.

Blogu hii pamoja na group la BINDA NEWS katika mtandao wa fb inatoa pongezi kubwa kwa ESTER BULAYA kwa dhamira aliyoiweka katika kutaka kulifanikisha hilo na kuwafanya vijana kushiriki katika michezo ambayo licha ya kupata burudani wanakuwa wanaibua vipaji na kujipatia ajira.

Ni agharabu kwa viongozi wengine wenye nafasi kama ya Ester ambao wako tayari kutumia sehemu ya kipato chao na kuwekeza katika michezo ambayo lengo lake si kujipatia fedha kapitia kile anacho kifanya bali kuhakikisha vijana wanajengewa uwezo kupitia michezo..

Blogu hii ipo tayari kutangaza mazuri yote ambayo yanafanywa na Mbunge huyu kijana ambaye imeonekana yupo katika nafasi hiyo kwa kuhakikisha yale yote yanayotakiwa kwa vijana yanafanyika ikiwa katika vikao vya Bunge ama nje ya vikao.

Usirudi nyuma na mwisho wa siku yale yote unayofanya ndio itakuwa dua njema kwako.

Post a Comment