0
BI BHOKE IDDY AMBAYE ANAENDELEA KUUGULIA MATATIZO ALIYONAYO NYUMBANI KWAO MTAA WA KENEDY MJINI MUSOMA NYUMBA NAMBA 77

ANAHITAJI MATIBABU MAKUBWA KWA MADAKTARI BINGWA MUHIMBILI MSAADA WAKO NI MUHIMU KWAKE

MAMA WA MGONJWA,MAMA DAMALI KONA AKIWA NA MJUKUU WAKE AMBAYE NI MTOTO WA BHOKE

AKIWA AMEJIPUMZISHA BAADA YA MAUMIVU MAKALI ANAYOYAPATA.
                                                     SOMA MAELEZO ZAIDI HAPO CHINI

Mama Damali Kona mfanyabiashara katika soko kuu Mjini Musoma anaomba msaada kutoka kwa wasamalia wema ili kuweza kumsafirisha binti yake Bhoke Iddy kwenda kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Mgonjwa huyo ameugua kwa muda mrefu na amekwisha pata matibababu kutoka katika hospitali ya Mkoa wa Mara na Bugando bila mafanikio na sasa amepewa rufaa ya kwenda Muhimbili.

Akizungumza na Blogu hii nyumbani kwake mtaa wa kenedy nyumba namba 77,mama Damali ameomba msaada kutoka kwa wasamalia wema na wenye muyo wa huruma ili aweze kujaribu kunusura maisha ya binti yake kwa madaktari bingwa.

Msomaji wa blogu hii kuwa na moyo wa huruma na msaada wowote utapokelewa na wahusika ili kufanikisha matibabu ya binti huyu.

Unaweza kupeeka msaada wako nyumbani mtaa wa kenedy nyumba namba 77 ama unaweza kuweka katika accaunti benki ya NMB A/C No 3031602562 au unaweza kuwasiliana na mama wa mgonjwa kwa simu namba 0754511991 ama kumtupia fedha kwa njia ya M-pesa.

KUWA NA MOYO WA MSAADA LEO KWAKE KESHO KWAKO.

Post a Comment