WAANDISHI WA HABARI WAKIPIGA KURA ZA MIKONO KUMALIZA TOFAUTI NA JESHI LA POLISI MKOANI Na Shomari Binda
Musoma,
Waandishi wa
Habari Mkoani Mara wameamua kumaliza tofati zao na Jeshi la Polisi baada ya
kuweka mgomo wa kuandika Habari kutoka katika Jeshi hilo tangu Septemba 11
Mwaka huu baada ya kuzuia maandamano ya kupinga kifo cha mwana habari Daudi
Mwangosi.
Maamuzi ya
Kusitisha mgomo huo umetolewa leo kwa kauli moja na Chama cha Waandishi wa Habari
Mkoani humo katika mkutano na wadau wa Habari uliofanyika katika ukumbi wa
uwekezaji wa Mkoa wa Mara.
Kamanda wa
polisi mkoani Mara kamishina mwandamizi wa jeshi la polisi Abslom Mwakyoma kupitia
mkutano huo amewaomba radhi waandishi wa Habari kwa tofauti zilizojitokeza na
kusema kuwa Jeshi hilo linawategemea sana waandishi wa Habari katika kufikisha
tofaoti mbalimbali katika jamii.
Alisema kama ni adhabu waliyotoa Waandishi wa
Habari kwa Jeshi la Polisi tangu Septemba 11 wamejifunza na kudai kuwa
watahakikisha tofauti zilizokuwepo zinamalizika na kufanya kazi kama timu
katika kuisaidia jamii.
Alisema hivi
sasa kumeibuka makundi ya wahalifu ya Mbio za vijiti,Mdomo wa furu,Jamaica mocas
na G5 ambayo yametishia amani kwa wananchi wa Manispaa ya Musoma na wakati
mwingine kusababisha mauji ya raia, hivyo alisema jeshi hilo limejipanga kukabiliana
na makundi hayo kuanzia sasa na kueleza bila ushirikiano na Waandishi wa Habari
hawawezi kufanikisha.
Kuhusu hatua
ya waandishi wa habari mkoani Mara kususia kuandika habari za jeshi la polisi kutokana
na kuzuiwa kwa maandamano hayo,kamanda
Mwakyoma,alisema hatua hiyo ilichukuliwa baada ya kubaini kuwa maandamano hayo
hayakufuata taratibu za sheria.
Awali katibu
tawala mkoa wa Mara Bw Clement Lujaji,akizungumza wakati akifungua mkutano
huo,amewaomba waandishi wa habari mkoani Mara kufanya kazi kwa kuzingatia
uzalendo pamoja na kuibua fursa zitakazo lenga kuchochea ukuaji wa uchumi wa
wananchi wa mkoa wa Mara.
Alitumia
nafasi hiyo,kuliomba jeshi la polisi na waandishi wa habari mkoani Mara,kuondoa
tofauti zao ambazo zilijitokeza na kusababisha kususiwa kuandikwa kwa habari za
jeshi hilo na hivyo kuwanyima haki wananchi kupata habari ambao ni haki yao ya
msingi.
Kwa sababu
hiyo waandishi wa habari wa mkoa wa Mara kwa kauli moja chini ya uenyekiti wake
Bw Emanuel Bwimbo,walitangaza kuondoa mgomo wa kuandika habari za jeshi la polisi
kuanzia sasa na kwamba wamemtaka kamanda wa polisi kukemea unyanyasaji ambao
umekuwa ukifanywa na askari wake dhidi ya waandishi mkoani Mara.
|
Post a Comment
0 comments