0

Mlinzi wa kampuni ya ulinzi ya salama iliyoko manispaa ya musoma ameuwawa kikatili kwa kuchinjwa shingo akiwa lindo katika pub inayojulikana kwa jina la tulivu na watu hao kuondoka na crate mbili za bia na viti .
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo kamanda wa polisi wa mkoa wa mara kamishina msaidizi Absalom mwakyoma alisema kuwa leo majira ya asubuhi eneo la majita road kata ya kamunyonge  manispaa ya musoma  mkoani mara  kwenye pbu tulivu uligunduliwa mwili wa john nyanganya  22 mlinzi  wa kampuni ya salama security ukiwa umekatwa shingo .

Mlinzi huyo alikuwa ameajiriwa kulinda  baa hiyo ya  na uchunguzi umeonyesha  kwamba  wauaji hao walivunja  pub hiyo ,baada  ya kumuua  na kuiba  crate mbili za bia  na viti vya plastiki saba na jumla ya vitu vinathamani ya shilingi laki moja na elfu sabini.

Mwakyoma alisema kuwa ufuatiliaji  wa kina  unafanyika katika kuwabaini  wahalifu hao waliofanya unyama huo  na kuwakamata.
Mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi akiwa na nondoo tatu ,mtarimbo pinde na mishale mitatu ,kirungu  na nguo za kike.
             

Post a Comment