0
Pendo Malima Mwanamke anayedaiwa kupigwa na mume wake

Waandishi wa Habari wakimchukua maelezo

Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Mara Beldina Nyakeke akichukua maelezo

Katimu Msaidizi wa MRPC naye alikuwa makini kupata taarifa

Mwana wa Afrika Augustine Mgendi naye alikuwa makini

Nami sikuwa nyuma

Ni kama anatabasamu lakini ungemsikiliza maelezo yake ungemuurumia



IKIWA Mkoa wa Mara unajiandaa na siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia bado matukio ya kupigwa kwa Wanawake yamekuwa yakijitokeza katika maeneo mbalimbali hali iliyopelekea Wananchi kutaka siku 16 ziwe za mafanikio katika kutokomeza hali hiyo.
Hivi karibuni Mwanamke aitwaye Pendo Malima (31) Mkazi wa Bohare Manispaa ya Musoma, Mkoani Mara alipoteza fahamu siku tatu baada ya kupigwa na Mumewe Ndege Aloyce ambaye ni Mvuvi kisa simu ya Mkononi.

Akizungumza na BLOGU HII Katika Hospitali ya Mkoa wa Mara wodi namba 4 alipolazwa Pendo alisema kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 17 mwaka huu usiku na kuongeza kuwa mume wake huyo amekuwa na kawaida ya kumpiga wastani ya mara tatu kwa mwezi.

“Ni kawaida ya mume wangu kunipiga mara tatu kwa mwezi kwani yeye ndio mwanaume ndani ya nyumba na mimi nakubali na kuona ni kawaida yake,”alisema Pendo.

Alisema kuwa siku ya tukio mume wake alifika nyumbani usiku na kumuomba simu yake lakini mwanamke huyo alimuambia kuwa atampatia simu hiyo siku ya pili yake asubuhi.

“Baada ya kumjibu hivyo aliamua kunipiga hadi nilipopoteza fahamu na kutojua kilichoendelea hadi siku ya tatu ndipo nilipopata fahamu,”alisema Pendo.

Alisema kuwa aliolewa na mwanaume huyo tangu mwaka 1996 na waliishi maisha hayo ya kupigwa lakini walifanikiwa kupata watoto watatu ambapo mkubwa anaishi na bibi yake na wawili anaishi naye.

Pendo alisema kuwa kutokana na kipigo hicho ajajua hadi sasa wapi ameumia ingawa alidai kuwa kichwa kinamuuma ingawa kwa sasa anaendelea vizuri.

Alisema kuwa baada ya kupatiwa matibabu na kupona ataondoka kwenda kijijini kwao Kiemba wilayani Butiama kwa kuwa amechoshwa na maisha ya kupigwa.

Alisema kuwa walishatoa taarifa Polisi na jeshi hilo linamsaka mtuhumiwa ili aweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili achukuliwe hatua za kisheria pamoja na kufikishwa mahakamani.

 Blogu hii inaahidi kushirikiana na Asasi ya ABC Foundation ya Mkoani Mara inayojishughulisha na Utetezi wa Haki za Wanawake na Watoto katika siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia zitakazoanza novemba 25 katika kata ya Bwiregi Wilayani Butiama.


Post a Comment