MABANGO MBALIMBALI YAKIPINGA UKATILI WA KIJINSIA |
KABLA YA MAMBO YOTE ILIANZA MICHEZO AMBAO TIMU YA WANAWAKE YA KITASAKWA ILIIFUNGA RYAMISANGA BAO 1-0 |
BAADA YA MICHEZO KAMANDA MWAKYOMA ALIKAGUA SHUGHULI MBALIMBALI ZA KINA MAMA WATAKA MABADILIKO |
BAADA ALIFIKA BANDA LA POLISI KITENGO CHA DAWATI NA KUPATA MAELEZO KUTOKA KWA MRATIBU WA DAWATI |
NAMI SIKUWA MBALI PAMOJA NA AHMAD NANDONDE WA VICTORIA FM |
IKAWA NI KUELEKEA ENEO LA MAZUNGUMZO NA WANANCHI |
NI MUHIMU KUSAINI KITABU CHA WAGENI |
MKURUGENZI NYARUGENDA NAYE ALISAINI KITABU CHA KIJIJI CHA KITASAKWA |
DC WA BUTIAMA MAMA ANGELINA MABULA NANE ALITOA NENO KABLA YA MGENI RASMI |
MKURUGENZI WA ABC FOUNDATION NYARUGENDA AKIBANJUKA HUKUAKICHANGIA UJENZI WA OFISI YA KIJIJI |
DIWANI WA KATA YA BWIREGI MWANA MAMA NYAGHETI ADAM AKIAGANA NA KAMANDA MWAKYOMA BAADA YA UZINDUZI |
Butiama,
JUMLA ya matukio 201 ya ukatili wa Kijinsia yamelipotiwa katika Jeshi la Polisi Mkoani Mara kutokea maeneo mbalimbali ya Mkoa huo katika kipindi cha mwezi Januari hadi Novemba Mwaka huu huku jamii ikitakiwa kubadilika na kukomesha matukio ya namna hiyo kuendelea kutokea katika Jamii.
Kauli hiyo
ilitolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani Mara Kamishina Msaidizi Mwandamizi
Absalom Mwakyoma alipokuwa akifungua kampeni ya siku 16 za kupinga Ukatili wa
Kijinsia kwa Wanawake iliyofanyika katika Kijiji cha Kitasakwa Kata ya Bwiregi
Wilayani Butiama iliyoandaliwa na Shirika la kutetea Haki za Wanawake na Watoto
la ABC Foundation Chini ya Ufadhiri wa Shirika la (WILDAF).
Alisema
idadi hiyo imeongezeka tofauti na mwaka uliopita ambapo katika kipindi cha
Mwaka jana matukio ya ukatili yaliyolipotiwa yalikuwa 148 huku watuhumiwa 51
walifikishwa Mahakamani na kati ya hao watuhumiwa 10 tayari wamekwisha hukumiwa
na wanatumikia adhabu zao gerezani.
Alidai
Mwanamke ni mtu ambaye anachangia kwa kiasi kikubwa katika Maendeleo ya Kijamii
ikiwemo kuchangia shughuli za Kiuchumi katika Jamii pamoja na kuwa mstari wa
mbele katika kuhimiza Elimu kwa Watoto kwa kuwa wao kwa asilimia kubwa ndio
wanaokuwa nao karibu hivyo anastahili kuheshimiwa na kupewa haki stahili.
Kamanda
Mwakyoma alieleza kuwa Binadamu wote ni sawa na wanastahili kutambuliwa na
kuheshimiwa utu wao hivyo ni wazi kwamba watu wote hususani Wanawake ambao
wamekuwa wakinyanyaswa kutokana na jinsia zao ni ukiukwaji wa katiba ya Nchi na
misingi ya Haki za Binadamu pale wanapofanyiwa ukatili.
Alisema
Jeshi la Polisi kupitia dawati la jinsia kwa kushirikiana na Asasi mbalimbali
zinazopambana na masuala ya ukatili wa kijinsia watahakikisha mapambano ya
kukomesha ukatili wa kijinsia Mkoani Mara yanakomeshwa hususani kwa Wanawake na
Watoto wanaofanyiwa Ukeketaji.
“Nimeajiliwa
kwa kufanya kazi na ntahakikisha nawashughulikia kwa mujibu wa Sheria wale wote
ambao bado wanaendeleza matukio ya unyanyasaji kwa Wanawake na Watoto pale
watakapobainika na sasa ni wajibu wa kila Mwananchi kubadilika na kuachana na
masuala hayo.
“Lazima
Mwanamke aheshimiwe na kila mmoja tusione ajabu leo kumuona Kamanda wa Polisi
akiwa mgeni rasmi katika uzinduzi huu kwa maana sasa tumeamua kwa dhati
kushirikiana na jamii katika masuala yote likiwemo suala la kupinga na
kukomesha unyanyasaji wa kijinsia na ndio iliyopelekea Mwaka 2007 ukaanzishwa
mtandao wa Polisi Wanawake na baadae Mwaka 2009 likaanzishwa dawati la jinsia
la Wanawake na Watoto,”alisema Kamanda Mwakyoma.
Awali katika
uzinduzi huo wa siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia,Mkuu wa Wilaya ya
Butiama Angelina Mabula aliwataka Wanawake kutokuogopa kutoa taarifa
zinazohusiana na masuala ya ukatili wa Kijinsia ili kila mmoja anaye husika
aweze kufikishwa katika vyombo vya Sheria ili hatua dhidi yao ziweze
kuchukuliwa.
Alisema
inahitajika mikakati madhubuti zaidi kwa lengo la kuondoa masuala ya ukatili wa
kijinsia kwani pamoja na kuwepo Sheria za kuzuia masuala ya ukatili bado
kumekuwepo na matukio kama hayo na kuwa kikwazo katika Maendeleo ya Wanawake.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Shirika la ABC Foundation,Eustance Nyarugenda alilishukuru
Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF) Kupitia
Shirika la Kivulini kwa ufadhiri wa siku
hizo 16 za kupinga ukatili dhidi ya Wanawake na kuahidi kuendelea na mapambano
dhidi ua ukatili hata baada ya kumalizika kwa siku hizo.
Post a Comment
0 comments