0
WAANDISHI WA HABARI KUTOKA JIJINI DAR ES SALAAM WAKIWA NA MENEJA WA TANRODS MARA EMANUEL KOROSO PAMOJA NA WANA HABARI WA MARA WALIPOMTEMBELEA OFISINI KWAKE

BAADAE WALITEMBELEA KATIKA BEACH MAARUFU YA MALTIVILA

Na Shomari Binda
        Musoma,

Waandishi wa Habari kutoka Clabu ya Dar es salaam City Press Clabu (DCPC) wamepongeza utendaji wa kazi unaofanywa na uongozi wa clabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Mara (MRPC) kutokana na kila kiongozi kuwajibika katika majukumu yake yanayomkabili na kuacha kuingiliana katika utendaji wa kazi na kumthamini kila Mwanachama.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa (DCPC) Joseph Kainga kwa niaba ya Viongozi na Wanachama wa Clubu ya Wandishi wa Habari kutoka Jijini Dar es salaam ambao wapo Mkoani Mara katika ziara ya mafunzo ya namna ya utendaji wa kazi wa Clabu za Waandishi wa Habari zinavyoendeshwa.

Alisema kutoka na taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa (MRPC) Emanuel Bwimbo wamependezwa na namna ambavyo kila kiongozi katika nafasi yake anawajibika kwa ufanisi bila kuingiliana na kumpa nafasi kila Mwanachama pale yanapotokea mafunzo mbalimbali ambayo yamekuwa yakitolewa na Muungano wa Clabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).

Kainga alisema ziara waliyoifanya imekuwa na mafanikio kwao kutokana na masuala mbalimbali waliyojifunza baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo makumbusho ya Baba wa Taifa Mwitongo Wilayani Butiama na katika viwanda na shughuli nyingine za kiuchumi.

Alidai Clabu ya (DCPC) kwa sasa ndio kama inaanza kutokana na kukumbwa na matatizo mbalimbali ya migogoro takribani miaka 6 hivyo jitihada zinafanywa ili kuirudisha na kusimama kama zilivyo clabu nyingine ambazo zimekuwa na ufanisi na uwajibikaji umekuwa ni wa wazi.

"Tumejifunza mambo mengi kutoka (MRPC) kwa muda wa siku tatu ambazo tumekaa hapa Mara na limekuwa ni somo kubwa kwetu yote tutaenda kuyafanyia kazi baada ya kufika Dar es salaam na tutamueleza kila Mwanachama kila kitu ambacho tumekipata katika ziara hii,"alisema Kainga.

Alisema wakiwa katika Makumbusho ya Butiama wamepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Madaraka Nyerere ambaye aliwaeleza mambo mengi kuhusiana na makumbusho hayo ambayo mwanzoni hawakuyajua vizuri lakini kupitia ziara hiyo wamepata kuyafahamu.

Kwa upande wake mmoja wa Wanachama wa (DCPC) ambaye yupo katika ziara hiyo anayeandikia Gazeti la MTANZANIA Arodia Pater alisema kwa yale waliyojifunza kutoka (MRPC) wanaamini yataleta mabadiliko makubwa katika kuimalisha clubu yao ambayo kwa sasa wana malengo ya kuiletea mabadiliko ya haraka.

Arodia ambaye pia ni mweka hazina msaidizi wa (DCPC) alisema amejifunza mengi namna (MRPC) wanavyofanya utaratibu mzuri katika udhibiti wa fedha ambapo uwazi unakuwepo na kila matumizi ya fedha yanayofanyika yanaingizwa katika vitabu na kila Mwanachama anao uhuru wa kuhoji katika Mkutano Mkuu wa clabu.

Wakiwa Mkoani Mara Waandishi wa Habari kutoka Jijini Dar es salaam walitembelea kiwanda cha Mara milk kinachotengeneza maziwa ya aina mbalimbali pamoja na maji ya kunywa,kiwanda cha samaki cha Musoma Fish pamoja na maeneo mbalimbali ya shughuli za kiuchumi.

Post a Comment