0
NIPO NA WADAU KUTOA ABC FOUNDATION TUKISUBILI MSAFARA WA CARAVAN WILAYANI TARIME

NDIO HIVYO WALIVYOFIKA NA KUWAPOKEA



MKURUGENZI WA ABC FOUNDATION YUSTUS NYARUGENDA KULIA AKIWA NA MWANASHERIA WA WiLDAF NEEMA MAKANDO BAADA YA KUWASILI

KIJIJINI MAGABIRI BAADA YA KUFIKA KATIKA VIWANJA VYA SHULE YA SEKONDARI MOGABILI

WAZEE WA KIMILA WA KATA 13 WILAYANI TARIME AMBAO KWA KIASI KIKUBWA WANAPINGA UKATILI WA KIJINSIA

NEEMA ALIYESIMAMA KULIA HUKU NYARUGENDA KUSHOTO WAKIFAFANUA JAMBO HUKU KAMANDA KAMUGISHA AKIWASIKILIZA

KAMANDA KAMUGISHA WA KANDA MAALUM TARIME RORYA AKISOMA HOTUBA

WADAU WA MABADIKILO



MAKAMANDA PIA WALIKUWEPO

NAMI SIKUWA MBALI KAMA MWANA MABADILIKO

NYARUGENDA AKIPOKEA KIASI CHA SHILINGI LAKI TANO KWA AJILI YA KUWAKABIDHI WAZEE WA KIMILA KWA KAZI YA MABADILIKO WANAYOFANYA

STAFF WA ABC FOUNDATION

Na Shomari Binda
       Tarime


IMEELEZWA kuwa Vyombo vya Habari hapa Nchini vimechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza matukio ya Ukatili wa Kijinsia kutokana na kuandika na kutangaza Habari ambazo zinaeleza athari za kufanywa kwa matukio ya Ukatili katika Jamii.

Kauli hiyo ilitolewa na Kamanda wa Kanda maalumu ya Kipolisi Tarime Rorya Justus Kamugisha alipokuwa akiitimisha msafara wa mabadiliko (CARAVAN FOR CHANGE) ambao umezunguka katika Mikoa mbalimbali ukiwa unatoa ujumbe wa kupinga masuala ya Ukatili katika Jamii Ulioanzia Jijini Dar es salaam Novemba 26.

Alisema vyombo vya Habari kwa kiasi kikubwa vimetoa mchango mkubwa katika kuhamasisha Jamii kwa kutoa taarifa mbalimbali zinazopinga na kukemea masuala ya Ukatili ambayo yamekuwa yakiendelea kutokea katika Jamii licha ya kuwepo kwa Sheria ambazo zinazuia mambo ya Ukatili.

Kamugisha alisema masuala ya ukatili yamekuwa yakikwamisha Maendeleo katika Jamii pale muanga wa Ukatili anaposhindwa kufanya kazi zake za kila siku za kujipatia kipato na kushughulikia matibabu ya Ukatili aliotendewa hali inayopelekea kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo.

"Jamii kwa kiasi kikubwa kwa kupata elimu kwa kupitia vyombo vya Habari imekuwa ikibadilika na kuachana na masuala ya Ukatili hususani Wilayani Tarime hivyo lazima vitambuliwe mchango wake katika kutokomeza masuala ya Ukatili mbalimbali katika Jamii,"alisema Kamugisha.

Alisema matukio ya ukatili mbalimbali uliolipotiwa Polisi katika kipindi cha Mwezi Machi 2010 hadi Februari 2011,kubaka yalikuwa 25,kukeketa makosa 5,mimba kwa Wanafunzi makosa 18 na kutorosha Wanafunzi makosa 14.

Kamanda Kamugisha alidai kuwa atukio yaliyolipotiwa Polisi katika kipindi cha kuanzia Machi 2011 hadi Februari 2012 makosa ya kubaka yalikuwa 18,kukeketa 1,mimba kwa Wanafunzi 7 na kutorosha Wanafunzi 7 ikiwa ni pungufu na makosa yaliyolipotiwa katika kipindi cha Mwaka 2010-2011 na kueleza kuwa bila msaada wa vyombo vya Habari huenda hali hiyo ingeongezeka.

Alisema licha ya Vyombo vya Habari,kupungua kwa makosa hayo ni pamoja na Elimu ya Polisi Jamii na Ulinzi Shirikishi kwa jamii inayotolewa kupitia Dawati la Jinsia ambapo askari wa kitengo hicho wamepata elimu namna ya kuwahudumia waathirika wanaoleta taarifa Polisi.

Kwa upande wake Mwanasheria wa Shirika la Sheria Wanawake na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF) Neema Makando alisema kila Jamii inapaswa kubadilika na kushirikiana kuhakikisha masula ya Ukatili mbalimbali yanakomeshwa na si kuyaachia Mashirika ambayo yanapingana na Ukatili.

(Ukatili unazigusa Jamaii zetu hivyo kila mwanajamii anapaswa kutoa ushirikianao ili lengo la kukomesha masuala ya ukatili mbalimbali yanakomeshwa il Jamii ikae huru na kuwajibika katika kufanya kazi za kujiongezea kipato na kupambana na changamoto nyingine za Maisha,alisema Neema.

Msafara wa mabadiliko (CARAVAN FOR CHANGE) baada ya kuzinduliwa Jijini Dar es salaa ikiwa na jumla ya watu 25 kutoka mashirika mbalimbali ya asasi za kupambana na masuala ya ukatili ilipita katika mikoa ya Kilimanjaro,Singida,Shinyanga,Mwanza na kuhitimishwa Mara Katika kijiji cha  Mogabiri Wilayani Tarime.
 

Post a Comment