0
MKURUGENZI WA ABC FONDATION EUSTUCE NYARUGENDA MWENYE BAHASHA AKIWAPOKEA WAGENI WA CARAVAN HII ILIKU NOVEMBA 30 2012 HUKO TARIME

HAPA AKIZUNGUMZA NA WAZEE WA KIMILA KATIKA UKUMBI WA MOGABIRI SEKONDARI HUKO TARIME

ANAKABIDHI SHILINGI LAKI TANO KWA WAZEE WA KIMILA KUTOKANA NA KAZI NZURI YA KUPINGANA NA VITENDO VYA UKATILI

ANATETA JAMBO NA MWANASHERIA WA WILDAF AMBALO NI SHIRIKA LA SHERIA WANAWAKE NA MAENDELEO BARANI AFRIKA NEEMA MAKANDO PAMOJA NA WANAHARAKATI WENGINE

MAREHEMU NYARUGENDA AKIWA KATIKA OFISI YAKE YA ABC FOUNDATION MJINI MUSOMA

NYARUGENDA NYUMA YA KAMANDA WA POLISI MKOANI MARA ABSLOM MWAKYOMA KATIKA UFUNGUZI WA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA HII ILIKUWA NOVEMBA 26 MWAKA HUU KIJIJINI KITASAKWA HUKO BUTIAMA
Na Shomari Binda
        Musoma

Mwanaharakati wa Shirika la la kutetea Haki za Wanawake na Watoto la ABC Foundation ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika hilo Eustace Nyarugenda (46) amekufa  katika kifo cha mashaka muda mfupi baada ya kufikishwa katika Hospitali ya DDH Mjini Bunda baada ya kutolewa katika nyumba ya kulala wageni akiwa hajitambui.

Katika taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari na Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mara Japhet Lusingu ilisema kuwa Marehemu alikutwa katika nyumba ya kulala wageni ya Savana katika chumba namba 4 akiwa anakoroma na kutoa povu baada ya kuvunja mlango wa chumba hicho alichokuwa amepanga Desemba 4.

Alisema katika chumba alichokutwa Mwanaharakati huyo ilikutwa chupa ya Bia mezani pamoja na dawa ya kuulia wadudu aina ya Nivan na uongozi wa nyumba hiyo ya wageni waliamua kuvunja mlango baada ya kupelekewa kitabu cha kusaini wageni na kusikia mtu akikiloma huku akishindwa kuitika.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa Marehemu aliondoka nyumbani kwake Musoma Tarehe 3 Desemba majira ya saa 12 asubuhi na hakuonekana kazini kwake wala nyumbani hadi alipobainika yuko Wilayani Bunda na mauti kumfika.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Mara alisema Marehemu alifariki muda mchache baada ya kufikishwa katika Hospitali ya DDH Mjini humo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Marehemu Eustuce Nyarugenda alikuwa Mwanaharakati wa kutetea Haki za Wanawake na Watoto katika Shirika la ABC Foundation na amekuwa mstari wa mbele katika mapambano ya kukomesha Ukatili mbalimbali unaotokea katika Jamii katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mara.

Kazi ya mwisho ya Kiharakati aliyoshiriki Nyarugenda ilikuwa Novemba 30 Mwaka huu Wilayani Tarime ambapo kupitia Shirika lake la ABC Foundation alipokea msafara wa mabadiliko (CARAVAN FOR CHANGE) uliokuwa na watu 25 kutoka Jijini Dar es salaam katika kuhamasisha kutokomeza vitendo vya Ukatili katika Jamii.

Jeshi la Polisi Mkoani Mara limesema linafanya uchunguzi wakujua chanzo hasa cha tukio hilo huku Kaimu Kamnda Lusingu akisema kuwa hadi sasa hakuna mtu yeyote ambaye amekamatwa kuhusika na tukio hilo.

Post a Comment