Jumla ya washiriki 80 wakiwemo wanaume hamsini na wanawake
ishirini wamejitokeza hadi kufikia siku ya jana tayari kwa kushiriki mashindano
ya mitumbwi ya BALIMI Mkoani Mara yatakayofanyika siku ya jumamosi katika fukwe
za Bwalo la Maafisa wa Polisi Mwisenge Manispaa ya Musoma.
Akizungumza na Blog hii,Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia ya
TBL Policalipo Makunja amesema kuwa watu
wengi wameendelea kujitokeza kujiandiksha katika Mwalo wa Mwigobero kwa Paschal
Matiku na inaonyesha mashindano ya Mwaka huu yatakuwa na ushindani mkubwa kutokana
na hamasa iliyopo.
Amesema hamasa nyingine ambayo imeongezaeka katika Mashindano ya Mwaka huu
ni kuongezwa kwa zawadi ambapo mshindi
wa kwanza kwa upande wa wanaume ataondoka na kitita cha shilingi laki tisa,wa pili laki 7,wa tatu laki 5,wa nne laki 4 huku mshindi wa tano hadi wa kumi wataondoka na kila mmoja shilingi laki mbili na nusu.
Kwa upande wa wanawake ataondoka na shilingi laki saba,wa pili laki sita,wa tatu laki tano,wa nne laki 4 huku mshindi wa tano hadi wa kumi kila mmoja kuondoka na shilingi laki mbili.
Poly amesema bado kuna nafasi kwa wale watakaohitaji
kushiriki mashindano hayo ambayo fainali zake zitafanyika Jijini Mwanza ambapo
wanaweza kujiandikisha kupitia kwa Paschal Matiku ama katika gari la
uhamashishaji wa mashindano hayo
lililoanza uhamasishaji tangu siku ya jana na leo jioni watakuwa na
uhamasishaji katika Bar ya Keryo garden Mjini Musoma.
Akizungumza sababu za kupeleka mashindano hayo katika Bwalo
la Polisi tofauti na mwalo wa Mwigobero ambapo yamekuwa yakifanyika kila
Mwaka,Poly amesema ni kupeleka burudani katika maeneo mengine lakini pia uwepo
wa kivuko cha katika eneo la Mwigobero pia ni sababu nyingine ya kufanyia
mashindano hayo katika fukwe za Bwalo la Polisi.
|
Post a Comment
0 comments