RAIS WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI TANZANIA (UTPC) KENETH SIMBAYA KULIA AKIWA NA MKURUNGEZI WA MUUNGANO HUO ABUBAKAR KARSAN KABRA YA KUKABIDHI VIFAA |
MAZUNGUMZO NA MAELEKEZO NI MUHIMU KABLA YA KUKABIDHIWA |
KATIBU MKUU WA KLABU YAWAANDISHI WA HABARI MKOANI MARA BELDINA NYAKEKE AKIPOKEA SEHEMU YA VIFAA HIVYO |
KATIBU MSAIDIZI WA MRAPC PASCHAL MICHAEL NAE ALIKUWEPO |
VIZURI EEEEEEEEEEEEH |
BAADAE MZIGO MZIMA ULIENDA STEND YA BUZURUGA MWANZA YALIKUFANYIKA MAKABIDIANO TAYARI KUJA MKOANI MARA |
MZIGO MZIMA UMEFIKA KATIKA OFISI ZA MRPC JENGO LA BODI YA PAMBA BARABARA YA MUKENDO MJINI MUSOMA |
UMEUONA VIZURI |
KATIBU AKIAANDIKA TAARIFA YA KUFIKA SALAMA |
BAADAE ULINGIZWA OFISINI |
Na Pascal
Michael Buyaga
Musoma
Jumla ya
shilingi milioni 800 zimetumika kununua vifaa vya vilabu 23 vya waandishi wa
habari Tanzania bara na zanzibar vilivyoanza
kutolewa jana na muungano wa
vilabu vya waandishi wa habari Tanzania UTPC kwa lengo la kuwaongezea ufanisi
wa kazi zao ambapo mikoa ya Mwanza ,Mara na Kagera imekuwa ya kwanza
kukabidhiwa seti 13 ya vifaa hivyo kila
mmoja.
Hafla hiyo ya makabidhiano ya vifaa
vya ofisi za klabu za waandishi wa habari Imefanyika jana katika ofisi za utpc jijini mwanza mtaa
wa isamilo ambapo rais wa utpc keneth simbaya
alikabidhi vifaa vyenye thamani ya milioni 105 kwa vilabu vitatu vya mwanza,mara na
kagera ambapo kila klabu thamani yake ni milioni 35 na kuwataka viongozi waliopokea vifaa hivyo kwenda kuvitumia kwa makini na si kuhoziwa na viongozi na badala yake wapange
mipango mikakati itakayowawezesha kujitegemea kwa kubuni miradi endelevu
Awali Rais alisema kuwa UTPC ilianzishwa kwa madhumuni ya kuimarisha vilabu vya
waandishi wa habari nchini ,kuchangia
kuleta maendeleo ya taifa sambamba na kuimarisha demokrasia nchini .
‘Ili
mwandishi wa habari aweze kufanya kazi
suala la uhuru ni muhimu sana ,ukibanwa utakuwa katika kipindi kigumu
ndicho tunachokipigania utpc alisema simbaya.
Alisema kuwa
vifaa hivyo vinalenga kuwa endelevu
katika kazi ambapo wanahabari
watafanya kazi kwa uhuru na kuhimili
matakwa yao ya kila siku tofouti na awali kuwazimu kuazima kwa baadhi ya wadau.
‘Sisi waandishi wa habari tunadhamana kubwa katika
jamii lakini matendo yetu hayaonyeshi taswira nzuri katika jamii ,tuwe
mfano katika jamii ili tuweze kuwa
kama mhimili wan ne wa serikali
alisema ‘’
Aidha alionya tabia ya baadhi ya waandishi wa habari walioanza kugawanyika kwa kuegemea upande
mmoja badala ya kuwa pande zote kwani
kazi ya mwandishi wa habari kuielimisha
jamii ili kuleta mabadiliko ya nchi kwa
kuikomboa jamii inayoteseka
vijijini na si kugawanyika kunakopelekea nchi kufika pabaya .
Vifaa
vilivyokabidhiwa ni seti 13 kwa
kila vilabu vilivyohudhuria hafla hiyo kila klabu imepatiwa destop computer ,printer ,laptop computer,ups
,binding machine,lamination machine ,photocopy machine ,multimedia projector,collapsible screen,professional
still picture camera,digital tape
recorder,dvd player na tv set.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa UTPC Abubakar Karsan
alisema kuwa historia kubwa imetimizwa ya ahadi ikiwa ni mojawapo ya Mkakati
wa kuimarisha vilabu ambayo tayari pia Mafunzo
mbalimbali yameshatolewa na utpc nia na madhumuni ni kuwajengea uwezo wanachama
wa vilabu ili kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa
Pia
amewashukuru wafadhili kutoka sida waliowezesha kufanikisha ufadhili huo
,hivyo vilabu havina budi kutowaangusha kwa kutumia vifaa hivyo kwa malengo
yaliyokusudiwa na si vinginevyo.
Wawakiishi
wa vilabu hivyo Wakiwemo wenyeviti wa
wawili kutoka kagera press club,mwanza press club na katibu
wa mara pres club ambaye ni Mjumbe wa bodi ya UTPC Beldina Nyakeke wameishukuru utpc kwa msaada huo mkubwa
na wameahidi kuvilinda na kuvitunza
vifaa kwani ni sehemu ya maisha yao
Post a Comment
1 comments:
no title tramadol for anxiety - tramadol 93 58