Na Shomari Binda Musoma,
Wanaharakati wa asasi
mbalimbali za Utetezi wa haki za Binadamu Mkoani Mara wametakiwa
kuendeleza harakati zao kwa kupigia kelele Sheria ambazo zimepitwa na
wakati na kuendelea kumkandamiza Mwanake hapa Nchini.
Wito huo
ulitolewa na muweseshaji wa Warsha ya mafunzo kwa watoa msaada wa
Kisheria na Watetezi wa Haki za Binadamu juu ya uelewa kuhusu Haki
Kisheria za Wanawake ,Desdevia Haule iliyoandaliwa na Shirika la
Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WiLDAF) iliyofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Kanisa la Anglican Mjini
Musoma.
Alisema zipo Sheria ambazo moja kwa moja zinamkandamiza
Mwanamke ikiwemo Sheria ya Mirathi ambapo kwa kiasi kikubwa
zinawanyanyasa Wajane na Watoto wa kike huku Sheria za Kilmila zikiwa
hazimtambui Mjane kama Mrithi wa moja kwa
moja.
Alidai katika Sheria hiyo Mjane Hurithi kupitia Watoto
wake na pia kanuni katika Sheria hiyo zinamchukulia Mtoto wa kike kama
mtu wa saraja la tatu baada ya Mtoto wa kiume huku Mtoto wa kiume
akiwekwa katika daraja la kwanza.
Mwezeshaji huyo aliongeza kuwa
mkataba wa nyongeza wa Haki za Wanawake Barani Afrika wa Mwaka 2003
ambapo Tanzania iliridhia mkataba huo mnamo Mwaka 2007 na kukubali kama
Nchi kubanwa na masharti yaliyomo lakini bado haki hizo hazitekelezwi.
Alisema
katika mkataba wa Kimataifa wa kuondoa aina zote za ubaguzi dhidi ya
Wanawake wa Mwaka 1979 ulioazimiwa na Umoja wa Mataifa Tanzania ni
sehemu ya utekelezaji wa mkataba huo.
"Baasdhi ya Haki ambazo
zimetakwa katika Mkataba huu na kuagiza Nchi husika kuhakikisha kuwa
hakuna ubaguzi dhidi ya Wanawake ni pamoja na haki ya kupiga kura (Ibara
ya 7),Utaifa (Ibara ya 9),(Elimu) ibara ya 10)Ajira (Ibara ya 11),Afya
(Ibara ya 12),Uchumi (Ibara ya 13 pamoja na
Ndoa (Ibara ya 16),"alisema mwezeshaji huyo.
Akizungumzia suala
la ukeketaji kwa Wanawake,Desdevia ambaye kitaaluma ni Mwanasheria
alisema jambo hilo ni udhalilishaji wa Mwanamke na kumshushia hadhi yake
hivyo kila Mwanaharakati anapaswa kupambana nalo na kuhakikisha
linakomeshwa Mkoani Mara.
Washiriki wa Warsha hiyo
inayofanyika kwa siku tatu itakuwa na mada mbalimbali ikiwemo Mikataba
na Maazimio ya Kimataifa kuhusu Haki za Binadamu za Wanawake,Sheria ya
Ndoa ya Mwaka 1971 pamoja na Sheria ya Aridhi Sura Na.113 na 114 za
Mwaka 1999 |
|
|
Post a Comment
0 comments